Nini tofauti kati ya maneno pesa na hela



Wewe umechanganya mambo meengi mno

Currency sio pesa ni ni sarafu
Coin sio lazima iwe pesa
Kuna coins za casino n.k.
 
Hela ni ile ya kubadilishia mboga na kunywea Serengeti lite, kama zile za MaK, Dangote wa madale, matajiri wa kinondoni etc.

Pesa ni kama zile za Mo, Bakhressa, Dangote wa Naija na wale Mabilionea wa majuu sio wa Njiro etc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
moyomacho tofauti pekee iliyopo ni kwamba, Hela zikiwa chache na Pesa zikiwa nyingi.
 
Fedha halali kwa malipo ya shilingi elfu kumi. Nadhani fedha ndo neno sahihi pesa na hela kitakuwa kinyantuzu
 
Hela unaweza nunua dagaa,kitunguu,sembe,kuni,mchele,unga,ndala,kiberiti,nyanya,nauli kwenye daladala nk

Pesa unaweza nunua range,Vx V8,buggatti,ferrari,Maghorofa,mademu wakali,anasa zote utakazo unaweza nunua wabunge nk .

Umeelewa hapo Mzee Brother?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji86][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23]we ndo mwalimu wa kishwahili. Nimeelewa Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kufahamu jinsi ya kutumia maneno yafuatayo:
- pesa
- hela

Mf: Alimpa pesa au alimpa hela

- ndivo ilivo au ndivyo ilivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app


Neno linalofaa ni alimpa pesa na sio Hela. Hela ni jina la pesa wakati wa utawala wa kijerumani hapa Tanganyhika na iliandikwa "Heller" hii ni sawa na pesa ilivyoitwa "shilling" katika utawala wa waingereza Africa mashariki.

Hivyo neno pesa, kwa kihindi "paise" ni sawa na neno money kwa kiingereza.

Neno fedha ni neno la kiarabu maana yake ni madini ya fedha au silver kwa kiingereza, jina hilo hutumika kwakuwa kuna baadhi ya Sarafu zilikuwa zimetengenezwa kwa hayo madini.
 
Naomba kufahamu jinsi ya kutumia maneno yafuatayo:
- pesa
- hela

Mf: Alimpa pesa au alimpa hela

- ndivo ilivo au ndivyo ilivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
pesa ni neno la kiswahili hela ni neno lenye asili ya kijerumani HELLER Ila yote maana ni ile ile.
Hela pesa lina majina mengi sana ya kimitaani kwa vile ni kitu kizuri
Ngawira, njuluku, mkwanja, mawe, kokoto, kakakuona.
 
pesa ni neno la kiswahili hela ni neno lenye asili ya kijerumani HELLER Ila yote maana ni ile ile.
Hela pesa lina majina mengi sana ya kimitaani kwa vile ni kitu kizuri
Ngawira,njuluku,mkwanja,mawe,kokoto,kakakuona,


Mkuu, neno sahihi hasa ni Pesa na sii Hela (Heller), Pesa ni sawa na Moneey katika kiingereza, Hela (Heller) ni sawa useme; Shilingi au Dollar, Pound sterling, Kwacha nk.

Hivyo neno sahihi kwa kiswahili ni Pesa na sio Hela, Shilingi, Fedha nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…