Nini tofauti kati ya maneno pesa na hela

The Most correct answer.
 
Sang'udi, Samahani kuuliza si ujinga. Kwenye hayo maneno hiyo Y imetokea wapi? Nijuavyo ni:
Ndio
Sio

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]
Hubadilika kulingana na ngeli itakayotumika
 
Mama mchungaji kwa kiswahili uko vizuri [emoji848][emoji848]
 
Pesa ni kiwango cha hela chini ya 100,000
Hela ni kiwango cha pesa zaidi ya 100,000
 
pesa ni neno la kiswahili hela ni neno lenye asili ya kijerumani HELLER Ila yote maana ni ile ile.
Hela pesa lina majina mengi sana ya kimitaani kwa vile ni kitu kizuri
Ngawira,njuluku,mkwanja,mawe,kokoto,kakakuona,
Pesa lina asili ya kihindi Paisa
 

Waziri wa hela
Waziri wa pesa
Waziri wa fedha

Hivyo, sio?
 
sarafu (currency) ya wakoloni wa kijerumani iliitwa heller, hivyo kwakuwa tuliitumia jina limebaki tunaendelea kulitumia kumaanisha fedha, pesa inatokana na wareno, nadhani wao fedha yao inaitwa peso, sisi tukaita pesa, kumbuka kuwa mreno aliwahi tawala pwani ya nchi yetu kabla ya waarabu wa omani kukita mizizi ya usultani wao pwani ya afrika mashariki.

kwa hiyo heller na pesa ni majina ya aina za currency zilizokuwa zikitumia na hao wageni walipokuja kutawala ila sisi tunatumia tu kuwa ni mbadala wa neno fedha

ni kama mtu akiamua kutumia neno rupia kumaanisha fedha (mfano: utasikia, penye udhia penyeza rupia, hapa rupia inamaanisha fedha , ila kihistoria ni fedha iliyoletwa na wakoloni wa kijerumani pia sultani wa zanzibar alileta rupia ya zanzibar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…