Nini tofauti ya muundo wa Jiji la Mwanza na Jiji la Dar?

Nini tofauti ya muundo wa Jiji la Mwanza na Jiji la Dar?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Mheshimiwa Rais Magufuli leo ametangaza rasmi mchakato wa kulifuta jiji la Dar ambalo linatokana na manispaa tano za mkoa wa Dar (Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni) ili kuunda jiji jipya (jiji la Ilala?) ambalo litatokana na manispaa moja tu ambayo ni ilala. Sababu kubwa aliyoitoa Rais Magufuli ni kuwa, muundo wa jiji la Dar uliopo sasa haustahili kuzijumuisha manispaa zote za mkoa wa Dar.

Sasa ukitazama jiji la Mwanza nalo linaundwa na manispaa mbili za Nyamagana na Ilemela. Muundo ambao unashahabiana na jiji la Dar pia.

Nini tofauti za msingi kwenye muundo wa majiji hayo mawili?
 
Jiji la Tanga linaundwa na manispaa ngapi?
 
Hakuna Manispaa ya Nyamagana bali kuna Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza lenye mipaka ya iliyokuwa Manispaa ya Nyamagana ambayo ilifutwa.
 
Hapa tunashindwa kuelewa, kwa mfano Mwanza mjini (kati) kuna wilaya mbili ambazo ni Nyamagana na Ilemela.

Ilemela imepewa hadhi ya kuwa manispaa ya Ilemela, lakini hakuna Manispaa ya Nyamagana badala yake Nyamagana imebeba hadhi ya Jiji la Mwanza.

Katika matukio yote ukisikia wanaongea jiji la Mwanza maana yake wanaongelea wilaya ya Nyamagana na sio mkoa wote.
 
Mimi nafikiri hii hoja imejikita zaidi kwenye mfumo wa utawala. Badala ya jiji la Dar-es-salaam kujitegemea kiutawala na kuwa na watumishi wapya tofauti na wale wa kwenye halmashauri zake 5 akiwemo mkurugenzi wa jiji la Dar-es-salaam, maafisa wa jiji la Dar-es-salaam na Baraza la madiwani wanaounda jiji la Dar-es-salaam. Pia kuwa na meya wa jiji ambao wote hao walikuwa kukilipwa mishahara na posho muundo huo unavyunjwa.

Badala yake halmashauri mojawapo ambayo ni Ilala imepandishwa hadhi ili kushughulikia mambo yote ya jiji la Dar-es-salaam.

Hivyo mkurugenzi wa halmashauri ya Ilala ndio mkurugenzi wa jiji kwa sasa, maafisa wake wote wamepanda hadhi kushughulikia masuala ya jiji.

Maana hata hapo mwanzoni ofisi za jiji la Dar-es-salaam zilikuwepo Ilala ila na watendaji wengine tofauti na wale wa halmashauri ya Ilala. Walikuwa wakijiendesha kwa kukusanya mapato ya halmashauri tano ikiwemo Ilala, Temeke, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni.

Ubunifu wa safu ya zamani ya jiji la Dar-es-salaam
ulikuwa mdogo na kuwa na idadi kubwa ya watumishi, hasa Baraza la madiwani likiongozwa na meya wa jiji ambalo lilikuwa lukilipwa posho kushughulikia masuala ya jiji. Baada ya vikao vya jiji wanatawanyika kwenda kwenye halmashauri zao tano tofauti na kujadili yaleyale na kuchukua tena posho za halmashauri hizo.

Kijografia inaonekana maeneo mengine ya Dar-es-salaam yatakuwa nje ya jiji lakini ukweli ni kwamba neno jiji mara nyingi huwa linabebwa na eneo dogo tu la kijografia kuwakilisha hadhi ya mkoa husika. Ila ukweli ni kuwa hata mwanzoni lilipokuwa linatajwa jiji la Dar-es-salaam, makao yake makuu na ofisi zake zilikuwa Ilala.

Hapo ni kwamba wafanyakazi wa jiji la Dar-es-salaam wa awali watapangiwa kazi nyingine. Ofisi itafungwa na shughuli zote zitahamia Ilala.
 
Jiji la Mwanza lilikuwa linaundwa na wilaya moja na baada ya kuligawa kuwa na wilaya mbili, wilaya ya Nyamagana ndio ikabeba jiji na Ilemela ikabeba hali ya kuwa manispaa
 
Hivi ndivyo alivyoamka leo!
Tukisema katibabya mwaka 1977 imempa rais mamlaka makubwa mno, kiasi kwamba kwa hisia zake tu anaweza kuamua atakalo na likaigharimu nchi, huwa tunamaanisha.
Tunataka katiba mpya
 
Tukisema katibabya mwaka 1977 imempa rais mamlaka makubwa mno, kiasi kwamba kwa hisia zake tu anaweza kuamua atakalo na likaigharimu nchi, huwa tunamaanisha.
Tunataka katiba mpya
Kichaa akiamka anaamua ataka yo . Lwa kweli maamuzi haya ya mtu moja yana athari kubwa sana kwa ustawi wa Yaifa letu na watu wake.

Tujiulize jee muundo huu wa jini la Dar ndio utaleta ustawi. Je huu ndio muundo wananchi wa Dar wanaotaka ?

Je majiji mengine duniani yanafuata mifumo kama hii ya kwetu?

Kkwa nini hatima ya Taifa la Tz iwekwe mikomoni mwa mtu moja tu?
 
Mheshimiwa Rais Magufuli leo ametangaza rasmi mchakato wa kulifuta jiji la Dar ambalo linatokana na manispaa tano za mkoa wa Dar (Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni) ili kuunda jiji jipya (jiji la Ilala?) ambalo litatokana na manispaa moja tu ambayo ni ilala. Sababu kubwa aliyoitoa Rais Magufuli ni kuwa, muundo wa jiji la Dar uliopo sasa haustahili kuzijumuisha manispaa zote za mkoa wa Dar.

Sasa ukitazama jiji la Mwanza nalo linaundwa na manispaa mbili za Nyamagana na Ilemela. Muundo ambao unashahabiana na jiji la Dar pia.

Nini tofauti za msingi kwenye muundo wa majiji hayo mawili?
Tofauti ni kubwa
 
Back
Top Bottom