Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Mheshimiwa Rais Magufuli leo ametangaza rasmi mchakato wa kulifuta jiji la Dar ambalo linatokana na manispaa tano za mkoa wa Dar (Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni) ili kuunda jiji jipya (jiji la Ilala?) ambalo litatokana na manispaa moja tu ambayo ni ilala. Sababu kubwa aliyoitoa Rais Magufuli ni kuwa, muundo wa jiji la Dar uliopo sasa haustahili kuzijumuisha manispaa zote za mkoa wa Dar.
Sasa ukitazama jiji la Mwanza nalo linaundwa na manispaa mbili za Nyamagana na Ilemela. Muundo ambao unashahabiana na jiji la Dar pia.
Nini tofauti za msingi kwenye muundo wa majiji hayo mawili?
Sasa ukitazama jiji la Mwanza nalo linaundwa na manispaa mbili za Nyamagana na Ilemela. Muundo ambao unashahabiana na jiji la Dar pia.
Nini tofauti za msingi kwenye muundo wa majiji hayo mawili?