Kubali kataa. Mimi ni mtanzania ila Kenya wametuzidi.
Angalia hata siasa zao, sasa hivi wanafanya kampeni lakini huwezi kuona wanavaa masare kama wanafunzi ndiyo ujue wapo katika Kujenga nchi mmoja.
Huku ni masare unajua kabisa hii nchi inamilikiwa na kikundi cha watu wachache.
Kwenye miradi ya wananchi ya watanzania wote bado mtu anavaa masare
Kipindi kile Raila Odinga alijiapisha kuwa raisi lakini aliitwa ikulu na Kenyata yakaisha lakini huku kutekana, kuuana na kusingizia kesi.
Ukiwa zako Kenya, unafanya business online unapata zako pesa kupitia Paypal maisha yanaenda. Hao jamaa wana NALA
Huo mshahara wa laki 5 ni wa kwenye makaratasi na bado makato