Na hapa ndipo kwenye tatizo kubwa! Mfano kama ningekuwa mimi ndiyo kocha; kwenye ile mechi ya jana, na hata zile mbili na Al Hilal, ningeanza na viungo wachezeshaji wote muhimu!
Mfano Bangala, Sure Boy, Feisal, na Azizi Kii. Halafu viungo washambuliaji wa pembeni kama Morrison na Moloko, wangeanzia nje! Kimsingi timu ina wachezaji wengi wazuri! Changamoto ni namna wanavyopangwa uwanjani.
Kwa kikosi kama hiki, Yanga haiwezi kusumbuliwa na Waarab kamwe; 1. Diarra 2. Juma Shabani 3. Kibwana Shomari, 4. Dickson Job 5. Bangala 6. Aucho 7. Aziz Kii 8. Sure Boy, 9. Mayele, 10. Fei Toto, 11. Farid Mussa!!