Ninyi viongozi wa umma mnaochapa watu viboko mnawachapa kwa mamlaka gani?

Ninyi viongozi wa umma mnaochapa watu viboko mnawachapa kwa mamlaka gani?

Hivi huko Tanganyika kwani mna sheria? si nasikiaga mnapewa "miongozo" na magufuli?

Yale matamko mbalimbali na AMRI za hapa na pale haziwatoshi tu?

By the way sheria za nini wakati mko na bulldoza jembe la majembe!?

Watanganyika kwa malalamiko hamjambo!
 
Hawako madarakani kwa kura halali za wananchi bali kwa nguvu ya dola, hivyo lazima watawale kwa shuruti na kuwadhalilisha wananchi. Isitoshe hiyo mahakama wameshainajisi hata wao hawana imani nayo tena, maana wamejua mahakama haina meno, hivyo wanajichukulia sheria mkononi kutokana na kuwa na madaraka ya kulevya. Hayo ndio madhara ya kuwa na serikali isiyo na ridhaa ya wananchi.
Katika mfumo wa kidemokrasia serikali huwekwa madarakani na wananchi kupitia sanduku la kura. Serikali inayotawala kwa uchaguzi usio halali, haiwezi wathamini wananchi.
 
Wewe umeona kuchapwa tu hujaona namna walemavu wanavyodhalilika!?.

Wanashinda juani kumbe wanamfanyia mtu kazi huku wao wakilipwa sehemu ndogo sana ya kinachopatikana.

Ingawa Serikali na yenyewe ni lazima ije kisayansi kwenye utatuzi wa suala hili.
 
Mi naona waendelee kupigwa mboko tu....wabongo hawasikii na wala hawaelewi...

kama walishindwa kumwelewa LISSU na hoja zote zile,...ngoja watandikwe viboko tu...hamna namn kwa kweli
Kwa kweli. Naunga mkono hoja.

Wacha watandikwe haswa. Hata mimi ningekuwa DC ningewatandika bakora kweli kweli.

Mijitu nyumbu nyumbu tu! Tandika kabisa.
 
It was Joseph de Maistre, the French philosopher, who said that in a “democracy, people get the government they deserve”.

Political cultures are generally a reflection of a society’s moral and social fibre. That’s why in some cultures you are flogged like a dog for committing a crime of moral turpitude.
 
Mimi napost ukweli ambao unaniuma sana. Katika karne hii, hata mnyama hapaswi kuchapwa viboko hadharani (maana kuna watetezi wa wanyama), lakini leo hii watanzania wanachapwa viboko hadharani na watawala, na watu tumekaa kimya au kulalamika kimya kimya mitandaoni. Nini tofauti yetu sisi watanzania na wanyama?

Watawala wametufanya sisi ni wanyama kwa kututandika viboko hadharani, na sisi tumelikubali hilo!
Ipo tofauti kati ya mnyama na Mtanzania. Wanyama kuna sheria za kuwalinda, kuna TSPCA. Watanzania wa kawaida, nje ya watawala, hawana mtetezi. Sheria zote zinatungwa na watawala kuwasurubu watawaliwa.
 
Tuseme ukweli ndugu yangu,hivi kupigwa viboko kumi hadharani na kuingizwa mahabusu ukaozee huko miezi mitano hadi sita huku DPP na hakimu wakikupiga danadana (DPP-Nategemea kubadilisha mashtaka,Hakimu-Leo hayupo anaudhuru) ni kipi bora?
Kuna watu wangeweza kumnasa makofi huyo waziri lakini busara inatawala wanaona ngoja waumie kidogo kwa muda mfupi kuliko ukaozeee rumande
Usipende kuandika ujinga kiasi cha kudhihirisha upumbavu na ujinga wako. Waziri anawachapa bakora kwa sheria gani? Mahakama hutoa adhabu kwa mujibu wa sheria. Huyu waziri ana mamlaka gani kutoa adhabu? Bora uende mahakamani upate adhabu halali kuliko kudhalilishwa.
 
Wewe utakuwa ni kati ya wapiga viboko. Mnairidhisha nafsi yenu, ipo siku mtalipia, hata kama vitakuwa ni vitukuu vyenu kusurubiwa na vyetu.
Upuuzi ni karama,hongera kwa kuwa na hiyo karama.
 
Ungekuwa wewe uulizwe kuchapwa viboko na kwenda jela unachagua nini? Ungesemaje,huoni kwamba kuchapwa viboko wamesaidiwa? Kwanini ukaanze kusumbua polisi na mahakama wakati unaweza ukawapa adhabu hapo hapo.
Kwa nini usikae kimya? Unaharibu bando lako bure.
 
hivi mtu akigoma inakuwaje kwamfano?
Atafunguliwa kesi ya kuzuia afisa wa serikali kufanya kazi yake. Baadae shitaka litabadirishwa na kuwa uhujumu uchumi, nyara za serikali au madawa ya kulevya. Na hapo ni baada ya kukaa ndani 48hrs kwa amri ya afisa wa serikali.
 
Mbona huu utawala wa awamu ya tano umegubikwa na mambo ya ajabu sana? Mbona tunaliabisha taifa letu?

Kama mtu ana hatia kwa nini asipelekwe mahakamani?

Sheria za hii nchi zipo wazi kuwa mtu anayepata adhabu ya corporal punishment lazima Dk athibitishe kuwa hawezi kupata madhara kama akipigwa viboko,pia adhabu hii lazima itolewe na mahakama.

Je kwa kihelehele chenu na kisabengo cha kupenda sifa mkipiga mtu akafa?

Mbona huu utawala wa awamu ya tano umekuwa na mambo ya ajabu na udhalilishaji?

Hivi Ccm hii inayojinasibu kuwa chama cha wanyonge ndio imekuwa ya kudhalilisha watu na kuacha kufuata sheria na katiba ya nchi!
WIZI WA KURA 2020 ULIPATA KIBALI TOKA MAMLAKA GANI??😃🤣🤣🤣
 
Mimi siku aje Boss wangu anichape viboko! Sitakubali zitapigwa mpaka tugawane nyumba za Serikali kama sio mimi basi yeye ataenda Polisi kuchukua PF3 akatibiwe Hospital na mwingine atalala mahabusu.
Kama ikitokea umeiba, yaani wewe ni mwizi na umekamtwa, nguvu hiyo ya kujibu kwa nguvu zote itapoteza labda awe akikuonea bila sababu.
 
Tuseme ukweli ndugu yangu,hivi kupigwa viboko kumi hadharani na kuingizwa mahabusu ukaozee huko miezi mitano hadi sita huku DPP na hakimu wakikupiga danadana (DPP-Nategemea kubadilisha mashtaka,Hakimu-Leo hayupo anaudhuru) ni kipi bora?
Kuna watu wangeweza kumnasa makofi huyo waziri lakini busara inatawala wanaona ngoja waumie kidogo kwa muda mfupi kuliko ukaozeee rumande
Yote hayo sio utaratibu.kupigana viboko na hivyo vitendo vinavyofanywa na Dpp vyote ni nivyakukemea.Nchi ya watu wenye akili timamu lazima izingatie misingi ya sheria na utawala bora.sasa ukiona tofauti na hivyo jua iko shida kubwa.Na tunavyoilea ndivyo inavyokomaa na iko siku itaturudi.
 
Ungekuwa wewe uulizwe kuchapwa viboko na kwenda jela unachagua nini? Ungesemaje,huoni kwamba kuchapwa viboko wamesaidiwa? Kwanini ukaanze kusumbua polisi na mahakama wakati unaweza ukawapa adhabu hapo hapo.
Kama ni hivyo mhimili wa mahakama, idara na taasisi zote zinazohusiana na kusimamia sheria na adhabu za makosa mbali mbali watumishi wake wapangiwe kazi nyingine.
 
Yote hayo sio utaratibu.kupigana viboko na hivyo vitendo vinavyofanywa na Dpp vyote ni nivyakukemea.Nchi ya watu wenye akili timamu lazima izingatie misingi ya sheria na utawala bora.sasa ukiona tofauti na hivyo jua iko shida kubwa.Na tunavyoilea ndivyo inavyokomaa na iko siku itaturudi.
Itabidi tuilee mpaka hapo watakapotokea watu wa ku sacrify kama Mwamwindi ndiyo watu watastuka.
 
Usipende kuandika ujinga kiasi cha kudhihirisha upumbavu na ujinga wako. Waziri anawachapa bakora kwa sheria gani? Mahakama hutoa adhabu kwa mujibu wa sheria. Huyu waziri ana mamlaka gani kutoa adhabu? Bora uende mahakamani upate adhabu halali kuliko kudhalilishwa.
Sawa,mie mjinga sasa kawachapa mbele ya DC wewe umechukua hatua gani?
 
Back
Top Bottom