Ninyi wanasiasa sio waaminifu kabisa mkipata madaraka mnawaza kufanya ufisadi,msipofanya mnajiona sio wajanja. Usikomae kuwaponda vijana

Ninyi wanasiasa sio waaminifu kabisa mkipata madaraka mnawaza kufanya ufisadi,msipofanya mnajiona sio wajanja. Usikomae kuwaponda vijana

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Nimemsikia Spika Ndugai akidai kuwa vijana wengi wa kitanzania sio waaminifu, kwamba wakiajiriwa mahala popote lazima wamuibie muajiri wake hivyo asipokuwa makini lazima wamfirisi. Unachosema ni kweli lakini hii mentality ipo kwa kiasi kikubwa hata kwa wanasiasa.

Wanasiasa wengi mpo kwa ajili ya kunufaika kwa dili za kifisadi. Mnapokuwa na madaraka makubwa kama yako nyie ni kutengeneza michongo ya ten percent ili mpige dili kubwa na msipopiga huwa mnajiona sio wajanja.

Sasa hivi umeanza kupigia chapuo mradi wa bandari ya Bagamoyo bila hata kutuambia kama mkataba una mapungufu na unahitaji marekebisho, umepiga chapuo kizembe sana kwa kudai uliikubali presentation ya Wachina wanaotaka kujenga Bandari Bagamoyo bila hata kuangalia madhara ya hao watu. Hii ni dalili tosha namna gani nyie wanasiasa huwa mnatetea mkate wenu wa ten percen bila kujali maslahi ya nchi.

Tumeshudia mengi hapa Tanzania, Escrow,Kagoda Epa Meremeta yote yakiwahusisha wanasiasa. Hivyo Spika kuwa mkweli,upigaji sio kwa vijana tu, hata wewe na wenzako.
 
Back
Top Bottom