Nioe mke mwingine?

Nioe mke mwingine?

Ahsante sana kwa mchango wako na ushauri wako mzuri, lakini suala la kukimbilia uhusiano mwingine huoni kama ni muhimu kwa kipindi hiki kwakuwa niko desperate na wakati huo yeye ana good time, think of mimi ndio nafanya kila kitu nyumbani (house boy) yeye anarudi muda anaotaka. Kwa sasa mtotot wake yuko boarding mimi wa kwangu yupo tunaishi naye nisipohangaika hali ni kweli niendelee kuvumilia? ya chumbani naogopa kusema nisijemvunjia heshima hapa mbele za watu.
Kwasababu mwenyewe unatambua kwamba uko desprate kaa ukijua kukimbilia mahusiano mapya katika hali hiyo sio vizuri.Unatakiwa usafishe akili yako na pia moyo wako...usitake kua na mtu kumkomoa huyo unaemuacha au ili ujione kwamba bado unaweza.Jitahidi sana urekebishe na kunyoosha mambo yako...kabla ya kuanza mahusiano mapya.Stress za kula/kulala na mtoto zinakutosha kwa sasa...subiri mpaka utakapo kua na amani moyoni mwako na utakapohisi sasa uko tayari kuanza na mtu mwingine kwasababu moyo wako kweli unahitaji hilo na hali yako nayo inaruhusu.Otherwise utakua humtendei haki huyo utakae kua nae maana utakua unamtumia tu kama ambavyo wewe umetumiwa...siku ukishapata unayotaka unamtupilia nae mbali!Kwavile tayari unayajua maumivu yake jitahidi kua muungwana usomsababishie mwingine!
 
Kuna mada ulikuja nayo hapa ukisema kama nakumbuka vizuri uamini ndoa. Kuna siku nikakushauri umtokee yule mheshimiwa wa kawe kwani yeye ataka mtoto tu si kuolewa. Kuna nyingine ulisema nyie medical doctors mna ethics. Sasa hii unasema wewe ni std seven. Anyway michango ni muhimu kwa wale wenye situation kama hiyo.
 
mambo ya kuachana sio mazuri,ila huyo m.ke si mke tena,haina haja ya vikao.kama vikao mmeshamaliza.ulimpenda na kumthamini ndio maana ukamsomesha.kwani ulijua wote ni wamoja.ukija kufanikiwa tena,atakuona wa maana.na jee ukiporomoka tena yatarudi upya.jee hayo ndio maisha ya ndoa?
 
ingawa una tatizo kubwa ila mimi kwa sasa sikushauri uoe, hebu pata kazi kwanza na umhudumie huyo mtoto wako..kibaya zaidi hujui huyo mke wa pili utakae mpata baadae atakuwaje ni kuomba heri tu..
siku zote tunasema tenda wema uende zako na msaada hauna risiti, hivyo basi wewe usihuzunike kumsaidia mke wako..Pole kwa yanayokukuta..
 
Pole sana ndugu,ikiwezekana mpeleke kwa wazee muyatatue kiutu uzima...hivi kwanini unapomsomesha mwanamke baadaye anakutenda?
 
ingawa una tatizo kubwa ila mimi kwa sasa sikushauri uoe, hebu pata kazi kwanza na umhudumie huyo mtoto wako..kibaya zaidi hujui huyo mke wa pili utakae mpata baadae atakuwaje ni kuomba heri tu..
siku zote tunasema tenda wema uende zako na msaada hauna risiti, hivyo basi wewe usihuzunike kumsaidia mke wako..Pole kwa yanayokukuta..

Spot on!
Nilikuwa nakuja kuandika jibu kama hili.

Mukama, badala ya bandika bandua, wewe lea tu mwanao wakati unauguza majeraha.
Sikushauri wakati huu ambao tayari ushaumizwa namna hiyo ukakurupuka kuongeza kiwanda kipya
cha matatizo. Uchaguzi wako hautakuwa makini.

Jipe muda kwanza,...nafasi nyingine ya kupenda na kupendwa ipo, Dont rush!
 
Pole sana ndugu,ikiwezekana mpeleke kwa wazee muyatatue kiutu uzima...hivi kwanini unapomsomesha mwanamke baadaye anakutenda?
Mkuu kuna actions zingine zinaonyesha mwenzako hakutaki, sio wazee wala uchawi utakaowarudisha pamoja...,
kumpeleka kwa wazee itakuwa mnapostpone the inevitable.., soon or later matatizo yatarudi, na mnaweza kujenga chuki na kufanyiana visa ambavyo mtajenga uadui wa maisha........
Na suala la kumsomesha mwanamke kwamba atakutenda nadhani halijawa proven tunahitaji data zaidi..., ila uwezekano unaweza kuwa kwamba sababu umemsomesha utataka kumtake for granted na kumfanya aone kwamba she owes you something
 
Duu poleeeeeeeee zakoooooooooooo
Ukiweza kampumzishe kwao kwanzaaaaaaaaaaa
 
Pole sana kwa yaliyokusibu.Usijilaumu kwa kumsomesha ni bahati mbaya hakutimiza malengo iliyoyakusudia wewe.Pia usigenerize kwamba wanawake wote ndio walivyo si kweli kwani kuna wanawake wameendelezwa na wamesoma sana na wakaendelea kuwatii na kuwaheshimu waume zao.
Kwa sasa jitahidi kujishughulisha uwe ili uweze kuwa na kipato chako,hata kama huna elimu unaweza kujishughulisha na biashara ndogo ndogo na Mungu atakusaidia utajikwamua kimaisha na kujiepusha na masimango na ulimbukeni wa huyo mkeo.
 
Huyu amekutema kama bazooka iliyoisha utamu mkuu. Wanawake wengi ni materialist, take it from me' kama hali ya uchumi ikiyumba kidogo unamwona anaanza kukuona huna maana na kama hela ikiisha kabisa na yeye anafanya kazi basi atakusulubu kabisa. Huwa sijui wameumbwaje hawa watu je wanafikiri mwanaume unaweza kuwa na hela kila saa bila hata upepo wa ukata kupita jamani. Akina mama mnatupeleka wapi? Mkuu usioe utaongeza pressure tulia uangalie kwanmza upepo unakwendaje na kumwomba Mungu kabla hujafanya huo uamuzi. ukioa mke mwingine mambo yanaweza kuwa yaleyela
 
Huyo mwanamke hakufai! Athari za kuendelea kuishi naye si tu zitakufanya ujione hufai lakini pia mwanao ataathirika kisaikolojia!

1.Achana naye; tafuta maisha yako mwenyewe.
2.Usikimbilie kuoa tena haraka; umesema huna pesa sasa, so unataka kuwa tegemezi kwa mwanamke mwingine?

Sahau na samehe, jipange anza moja; na utafanikiwa kwa yote!
 
Mkuu pole sana,usikrupuke kuoa nyumba ya pili hakikisha unatafuta mradi wa kufanya kwanza.
Ukiona majaribu yamezidi ujue wokovu unakaribia
 
Pole sana mkuu kwa mtihani huu ulionao...nakushauri upige goti uzungumze na Muumba wako.
 
Hapo kaka kwanza tuliza akil yako ili ujue nini cha kufanya baada ya kutengana na uyo mkeo. kuoa tena si suruhu kwanza tafuta maisha ya uyo mtoto wako.
 
Ndugu zangu naombeni msaada kwenye kisa hiki cha kweli . nina mke tuliyefunga ndoa yapata miaka 11 iliyopita, mke wangu tulikutana kazini kwenye kiwanda cha kutengeneza biscuits ambapo yeye alikuwa teller mimi ni mwendesha mashine.
Baada ya kuoana nilimwendeleza kimasomo kwakuwa yeye alikuwa wa form IV nami ni darasa la saba, kwakuwa alifanya vizuri katika kozi zake alifanikiwa kupata kazi kwenye shirika moja la kimataifa kama administrative secretary.
Sisi huku kiwanda kilifungwa kutokana na biscuits kukosa masoko kutokana na ushindani uliopo hivyo nikalazimika kukaa nyumbani huku nikijitahidi kutafuta vibarua vya hapa na pale.
Issue ni kwamba mke wangu sasa amekuwa mbogo hataki kusaidia kitu chochote hapa nyumbani na ikitokea akatoa hela basi masimango yanatisha, tutaitwa majina ya kila aina mara poyoyo, mara Mario nk.
Wakati tunaoana kila mmoja alikuwa na mtoto na wote tulikuwa tunawalea kwa mapenzi bila ubaguzi, cha kushangaza yeye mtoto wake kampeleka international school wa kwangu amemwacha aendelee na hizi za kayumba!
Kinachonipa taabu sana ni kurudi usiku wa manane wakati mwingine akiwa amelewa nikimuuliza anasema walikuwa na kazi nyingi na mikutano inayoambatana na vinywaji, pia ana safari nyingi za kikazi na akifika huko huwa hataki nimpigie simu eti namsumbua!
Sasa je huyu bado anastahili kuwa mke wangu? Si kawa wa mataifa sasa niachane naye nikaoe mwingine?
Vikao vya wazee vimeshindwa kutoa ufumbuzi wanamuogopa au sijui ni kwamba anawakatia mkwanja mrefu?!
Nawasilisha
Pole sana mwenzetu,maisha ndivyo yalivyo na wewe si wa kwanza kuumizwa kiasi hicho,piga moyo konde,vumilia maumivu kisha songa mbele ie tafuta shughuli yoyote ya kukupatia kipato.Kwa sasa usichague kazi,ilimradi iwe ya halali na mkono uende kinywani.Dhana ya kwamba kwa kuwa ulimsomesha alipe fadhila IFUTE AKILINI MWAKO!Ndiyo inayokudumaza hata unaishia kukaa nyumbani muda wote,na kwa kuwa unakuwa hapo huwezi kwepa majukumu madogomadogo ya hapo hasa ukuzingatia una mtoto asiye na mlezi zaidi yako kwa sasa.Pia ondoa dhana kwamba kazi za nyumbani hufanywa na housegirls tu!Kwani wakati unaishi kwenu hukuwa unamsaidia mama yako kazi za nyumbani??(Kama haikuwa hivyo,hayakuwa malezi mazuri). Jione kwamba wewe ni single parent at least for now,ili uyabebe majukumu kama mzazi na usilaumu.Umizwa kichwa kutafuta maisha yako na future ya mtoto wako,SIKU isiyojina mambo yatabadilika KAMA unamtanguliza Mungu katika kila ufanyalo.Pole sana,Hakika inaumiza!
 
mkuu pole kama ni kweli
ningependa kujua hiyo nyumba mmepanga au ni yenu
vyovyote vile hama muage vizuri mtoto mhamishie kwa wazazi au nduguzo
hamia mkoa mwingine katafute kazi au anza biashara
kama ana chembe ya mapenzi atakutafuta
kama hana atajuta kumkosa houseboy na hiyo utaiona wakati mkiwasiliana
kwa yeye kukaa mwenyewe na wewe kuwa mwenyewe utaweza kuwa free thinking
usikimbilie kuoa kwanza tafuta pesa si unajua "ukitafuta wanawake utapoteza pesa ukitafuta pesa wanawake watakufuata"
ukikaa mwenyewe kwa miezi mitatu mpaka sita utajua ukweli ingawa hilo suala la kutoa mimba ina maana hapo future hakuna ila kaa mwenyewe kwa muda pata kazi wakati hujamuacha officially then ukitulia utakuwa na maamuzi ya busara
 
Kuna mada ulikuja nayo hapa ukisema kama nakumbuka vizuri uamini ndoa. Kuna siku nikakushauri umtokee yule mheshimiwa wa kawe kwani yeye ataka mtoto tu si kuolewa. Kuna nyingine ulisema nyie medical doctors mna ethics. Sasa hii unasema wewe ni std seven. Anyway michango ni muhimu kwa wale wenye situation kama hiyo.

Nashangaa kuna watu wengine wanaleta mastory ya uongo hapa...
 
Kwasababu mwenyewe unatambua kwamba uko desprate kaa ukijua kukimbilia mahusiano mapya katika hali hiyo sio vizuri.Unatakiwa usafishe akili yako na pia moyo wako...usitake kua na mtu kumkomoa huyo unaemuacha au ili ujione kwamba bado unaweza.Jitahidi sana urekebishe na kunyoosha mambo yako...kabla ya kuanza mahusiano mapya.Stress za kula/kulala na mtoto zinakutosha kwa sasa...subiri mpaka utakapo kua na amani moyoni mwako na utakapohisi sasa uko tayari kuanza na mtu mwingine kwasababu moyo wako kweli unahitaji hilo na hali yako nayo inaruhusu.Otherwise utakua humtendei haki huyo utakae kua nae maana utakua unamtumia tu kama ambavyo wewe umetumiwa...siku ukishapata unayotaka unamtupilia nae mbali!Kwavile tayari unayajua maumivu yake jitahidi kua muungwana usomsababishie mwingine!

Ni kweli usemayo lakini jamani hivi kweli mimi sina haki ya kuliwazwa katika magumu haya?!, mwenzangu ana ponda life yaani kanisahau kabisa, pia kuna suala la kimwili ambalo sijalisema hapa namimi ni mtu mzima niliyekamilika sana kijinsia navumilia kutopata haki hii kwa muda mrefu wakati nahisi mwenzangu anapata ndio maana hana tena shida na mimi.

Nakula kwa kufanya vibarua vya kazi ndogo ndogo si kama mimi na mtoto tunamtegemea yeye keshatubwaga kabisa! hasa ukizingatia kuwa wa kwake yuko boarding.

Pia tusisahau kuwa ajira zenyewe ni taabu siku hizi hata kwa wasomi wenye shahada zao kwangu nikisubiri kujijenga si nitazeeka manake inabidi nirudi shule ili nipate kazi.

uamuzi wa kutafuta mwingine nimeufanya kwa mpangilio kwa mfano nilipojiunga na jf ilikuwa njia mojawapo ya kutafuta faraja kwa kubadilishana mawazo kama hivi, ndio maana utaona sikulisema hili mwanzo mpaka nilipoelewa utaratibu wa mada zinavyowasilishwa.
kwa hiyo nitakayempata atajua nimekosa nini huko kwa awari na tutazungumzia uwezekano wa mapenzi ya dhati kabla ya kupiga hatua zaidi.
 
Back
Top Bottom