Niokoeni jamani nimeanza kumpenda Mzigua90

Niokoeni jamani nimeanza kumpenda Mzigua90

Haya mambo ya thread thread sio ishu, nenda pm mwambie "bibie nna kisalio hapa nataka nikutumie upate lunch , sijui niitume vipi mama" Mzigua90 nae ana moyo lazma moyo utalegea atakupa namba ukifanya muamala itapendeza, hadi hapo mpira upo ndani ya box. Mnakompliketisha mambo
Sasa hii thread itaishia kukupa likes tu
Ameeeeeeèen mama. Kama asipoelewa huu ushauri basi tena.
 
Chunga sana @Aspirin anakusikia
Ndondondo si churururu ! Ndivyo ilikuwa nianza kwa kupenda michango yake iliyopevuka iliyosheheni mapenzi ya kweli na nia ya utulivu uso kifani,Taratibu dozi ikaanza kuniingia lahaula la kwata nikajaa nikawa bingwa wa kufuatilia post zake kuliko hata navyofuatilia za mshana jr ,deo msando na gudume .

Najileta kwenu waungwana mninusuru kwani nishaona dalili kuwa mzigua90 ataninyanyasa sana kwani mtizamo wake juu ya mahusiano ni hasi na ni dhahiri ni mtu mtemi asieshaurika, na ukiweka na kauzigua (Tanga ndo yalikozaliwa) mimi mnyalu wa watu najiona nikiuza kiwanja cha urithi.

Nafwaa wajameni.
 
Tatizo la vijana siku hizi mnataka shortcut sana. Huku tunaita uoga uliokithiri. Kwann usimtafute bila kutoa thread? Hii thread ilifaa iandikwe hivi.
Nashukuru ndoto yangu ya siku nyingi imetimia. Huyu mwanamke niliona mchango wake JF nikatokea kumpenda na hatimaye ndoa yetu itafungwa tarehe 2 feb 2018. Kadi za harusi zipo kwa mawasiliano zaidi 071xxxxxxxxx
Wanaume kama wewe ndo nawapenda
 
Hivi kwanini sisi Wanaume Tunapenda Penda Hovyo Watu Tusio Wajua? Wewe Limtu Hulijui Hujawahi Liona Wala Kulisikia Sauti Afu Unajikuta Tu Unalipenda Khaaaa! Utapenda Majini Mzee Baba.
Ndo kutake risk huko jamani
 
Back
Top Bottom