Miaka ya themanini wakati TZ inaisaidia Frelimo dhidi ya waasi RENAMO, Siku moja msafara wa Jeshi kutokà TZ baada ya kusafiri kwa Siku kadhaa walipumzika porini, kumbe wameuzwa, taarifa za kupumzika pale zimepelekwa kwa waasi mapema, na wale waasi walikuwa wanawasubiria pale wakiwa kwenye mahandaki,
Wakati wanapumzzika walitoka kwenye magari yao kwa ajili ya chakula na kutembea tembea, ghafra walishangaa risasi zinamwagwa Kama mvua toka kila upande, njia pekee ni kujificha kwa kupotea ghafra!, japo mwisho wangetekwa tu sababu walisha zungukwa.
Askari mmoja aliyekuwa ameokoka, alikuwa anaendesha kifaru alikipaki chini ya mti mkubwa, na kifaaru chenyewe kilipambwa na miti hivyo kuwa Kama kichaka, yeye alikuwa Kama mita 100 toka kwenye kifaru, askari wenzie walipojificha alijua watakamatwa tu, akaamua kukimbilia kifaru chake, kwa hiyo yeye peke yake akawa anakimbia anaonekana na wale waasi, na ni sehemu ya wazi, hivyo risasi zote za waaasi zikaelekezwa kwake, kumbuka watu zaidi ya 100 wanamwagia risasi mtu mmoja, hakuna iyompata.
Alipoufikia ule mti aliurukia na kudumbukiq ndàni yaa kifaru, mlango wa kifaru ni tundu lipo juu, waasi waliukausha ule mti kwa risasi kwa sekunde chache. Ikawa ni zamu yao kushangaa kuonà kichaka kinatembea, wote waligeuzwa vipande vya nyama. Ndio akaanza kuchomoka askari mmoja mmoja alikojificha,, na kushangaa jamaa alikwepaje risasi, YESU YUPO HAI