Wao wanaenda kupigana kwa faida ya raia wa Tz pia.
Labda nikuuluze swali ambalo jibu lake litakupatia mwanga kidogo kuhusu faida yake.
Ukiwa na jirani mkorofi, mshari, mgomvi sana, leo kaja kutinga nyumbani kwako, umemsikia tu anatukana kishari, lakini kabla hajaingia ndani kwenye compound yako, ni maamuzi gani ya haraka unayoweza kuyachukua ili asijekuingia ndani na kukusababishia hasara kubwa?
Kama jibu litakuwa ni kumfuata huko huko nje ili mkamalizane, basi jibu hilo ndiyo mfano wake hutumika kumfuata adui aliye nje ya mipaka ya nchi kwenda 'kufanyiziana' naye huko huko ili kuhami maisha na ustawi wa raia wetu.
Pamoja na madhumuni ya jeshi uliyoyataja kwa kimombo, lakini kumbuka kuwa nchi nyingi za kusini ya mipaka ya Tz, ukombozi wa nchi zao, umepatikana kwa majeshi ya Tz kujiinguza moja kwa moja kijeshi ama kuwafadhili na kuwapa hifadhi wapigania uhuru wa mataifa hayo.