Nionavyo mimi: Miaka kumi ya Rais Magufuli umasikini utaongezeka sana

Hapa kuna mambo tofauti, ujenzi wa miundo mbinu, kuimarisha uwajibikaji kisheria mfano kupiga vita rushwa na mwisho kabisa ni ukuaji wa uchumi

Aspect ya mwisho ya ukuaji uchumi ni dependent variable na inaathiriwa chanya na hasi na masuala ya miundo mbinu, utawala wa sheria,uwekezaji (wa nje & ndani).

Tulio wengi HATUJUI mahusiano ya ukuaji wa uchumi (micro & macro) na hiyo miundo mbinu inayojengwa.

Kwa sasa miradi mikubwa haijakamilika hivyo return yake bado huwezi kuiona kwenye pato la Taifa/GDP ndio kusema hizo ni longterm investment.

Ambacho wengi tunakurupuka ni kutokuona hali halisi ya haya mambo, jiulize:

- Je sekta binafsi imekua au imevurugika kabisa tangu awamu hii iingie madarakani?

-Vipi wawekezaji wakubwa kutoka nje hali ikoje (vipi foreign direct investment FDI)

-Hali ya uchumi kwa mtu ie economy at micro level ikoje?

-pato la mtu ie per capita limepanda au limepungua?

Mwisho- vipi fursa za ajira (public & private sector) hali ikoje?

Majibu au mtazamo wa ndani wa hayo hapo juu ni baadhi ya viashiria vya hali ilivyo.

Mnaosema uchumi umepanda au kushuka bila kuzingatia hayo na mkahisi labda barabara daraja au reli ndio kiashiria cha kukua uchumi, mtakua mnachanganya utekelezaji wa ilani ya chama na kukua au kushuka kwa uchumi wa nchi!
 
Sasa unachopinga ni kipi? Basi tuambie wewe unaejua serikali imenunua korosho kwa bei gani? Na kuhusu watu ambao hawajalipwa shida sio serikali ni viongozi wa vyama vya msingi ndio ambao wanaleta ubabaishaji hasa makatibu wa vyama vya msingi ndio maana wiki kadhaa zilizopita akatangaza kuvivunja na kuvifutia usajili baadhi ya vyama.
Mimi ni miongoni mwa watu ambao nilipima tani kadhaa lakini nikazungushwa kwenye malipo lakini nikaamua kufuatilia mwenyewe kuanzia wilayani matokeo yake wiki tatu zilizopita pesa zangu zikaingizwa kwenye Akaunti tena kwa bei ileile ya 3300.
Tunawaomba nyie chadema kwenye msimu wa Korosho ujao korosho muje muzinunue nyie japo kwa TSH 3000 ili muwanufaishe wakulima
Acheni kuuongopea Umma.
Hongera JPM naipenda Tanzania
 
Kumbuka wakati huyo Magufuli ananunua korosho ya mkulima kwa bei hiyo, tayari kulikuwa na rekodi ya korosho kuuzwa kwa bei zaidi ya Sh 4000. Lazima Alaumiwe kwasabu korosho ilishuka thamani tofauti na ilivyotarajiwa.
Kwa hiyo kama kulikuwa na rekodi ya korosho kuuzwa TSH 4000 haiwezekani bei kushuka? Hivi unafahamu sababu ya serikali kuchukua jukumu la kununua korosho. ?
 
Wakulima wengi wamelipwa 2640/= na kuna baadhi wamerudushia korosho zao hasa wale wa Newala na Naliendele-Mtwara.

Sasa huoni ulivyokuwa zumbukuku unajisifia kulipwa fedha za korosho mwezi huu wa 5 mwaka 2020, na ni korosho ambazo uliuza mwaka juzi?

Hivi kwa akili zako za MATAGA, hiyo fedha ambayo umelipwa wiki 3 zilizopita ni sawa na mtu aliyelipwa Tzs 3000 mwaka juzi ki-thamani? Mwaka huu umeshasikia malalamiko kuhusu malipo ya korosho?

Embu tuambie wewe kama Serikali ilikuwa inalipa moja kwa moja kwa mkulima hao Makayibu vya vyama vya Msingi wana kosa gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo kama kulikuwa na rekodi ya korosho kuuzwa TSH 4000 haiwezekani bei kushuka? Hivi unafahamu sababu ya serikali kuchukua jukumu la kununua korosho. ?
Aliyechukua jukumu la kununua korosho alikurupuka na ndio maana mpaka leo ameshindwa kulipa watu fedha zao, alifikiri ni sawa na biashara ya Ice cream.

Ungekuwa na mawasiliano na Kabudi, Bashungwa na Mwambe wangekuambia kuhusu korosho na waliyokutana nayo baada ya kuweka matarajio makubwa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ninachojali pesa yangu nimelipwa haijalishi ni lini.
Wakulima inapaswa wajilaumu wenyewe sababu wanunuzi kutoka India na Vietnam walitaka kununua korosho kwa TSH 2500 wao wakakataa kuuza wakisema bei ni ndogo wakaiomba serikali iwasaidie sasa wewe ulitaka Magufuli afanye nini?
 
Kwani ilikuwa lazima afanye maamuzi aliyafanya? If yes Mbona mwaka uliofuwata hakurudi tena? Bad advice ndio maana mwaka uliofuwata hamkuleta jeshi tena. Ingekuwa ni wazo zuri msingeacha rudi kununua tena.
 
Umeongelea mambo mengi Ila umesahau stahiki za watumishi wa umma. Hakuna increment wala kupanda madaraja kwa kipindi cha miaka mitano. Pamoja na hayo yote bodi ya mikopo imeongeza makato kutoka % 8 mpaka% 15 nje ya mkataba ambao watu walisaini kipindi wanaomba mikopo. Pamoja na kuongezeka Kwa makato ya HESLB pia zimeongezwa faini mbalimbali kwenye ambazo zinapeleka watumishi kwenye dimbwi la umasikini.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani ilikuwa lazima afanye maamuzi aliyafanya? If yes Mbona mwaka uliofuwata hakurudi tena? Bad advice ndio maana mwaka uliofuwata hamkuleta jeshi tena. Ingekuwa ni wazo zuri msingeacha rudi kununua tena.
Hili sio jibu la swali ambalo nimeuliza.
Hawajarudia kununua kwa sababu wakulima hawajasusa kuwauzia Wahindi ila wakisusa Magufuli atanunua tena.
Hongera JPM naipenda Tanzania.
 
Wenyewe wakija hapa watakujibu mambo ya SGR,Stigler's gorge,kujenga zahanati kila kata,elimu bure etc

Ndio majibu yao hayo,waulize sasa haya mliyoyasema yanamsaidiaje mtumishi wa umma?Utasikia nyie ni wapiga dili tu.
 
Wakati ule alikuwa mgombea Uraisi kwa tikiti ya chama chenu alikuwa msafi?

God save us
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…