Nionesheni bodaboda aliyeagiza gari Japan au China kwa kipato cha bodaboda niache kazi ya utumishi wa umma ndani ya saa 24

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hii sasa ni too much

Unamfananishaje mtu anayekufa kama nzi hapa jijini Dar es Salaam na mtumishi wa umma?

Unamfaninishaje bodaboda ambaye akipata ajali kubwa tu anakimbizwa Kijijini kwa mama yake akafie huko na mtumishi wa umma ambaye ana bima ya watu 6?

Mtu akistaafu anakunja mpaka milioni mia moja leo hii unamfananisha na Bodaboda ambaye hata nywele kuchana ni mtihani.

Nionesheni bodaboda mwenye nyumba angalau ya milioni 20 ambayo Kajenga kwa kazi ya kubeba watu?

Sasa hivi muda wa kazi ukipita ofisi za umma zikiwemo shule za msingi Dar es salaam utakutana na gari namba C,D na E nyingi za walimu na hazijawahi kukosa mafuta hata siku moja.

Na service zinafanyiwa kwa wakati. Bodaboda akiharibikiwa cylinder head ya 35 anahangahika kama kaibiwa figo
 
Unafundisha shule gani mkuu?
 
Mimi sio mwalimu ila ni mtumishi, kuna walimu nimewazidi maslahi na wengine wamenizidi , naishi vizuri tu.
Bodaboda wote mtaani wananiheshimu.
Kwanini muwakebehi walimu kiasi hichi?
Achana nao mkuu....huenda dharau zao zatulisha....sisi tunawapa ushindi tu watukane watakavyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…