Nipe sababu tatu unapenda kuishi ukanda gani mwa Tanzania?

Mzee wa fisi kwema?tukutane hapo paris
 
Nimezaliwa na kukulia ukanda wa Pwani nimesoma Dodoma, Iringa na Mtwara yaani O Level, Chuo na Advance, kwa Mtwara shule ni hapo Ndanda ulipopasema. Vijiji vya Mwena, Mkalapa n.k Vibe la Dar tangu nikiwa mtoto. Nimeishi nikifanya kazi Mwanza mjini. Nimefika Geita, Musoma, Mara mpaka Sirari, Kahama, Simiyu hasa Bariadi bila kusahau kisiwani Nansio, Ukerewe kupitia Bunda.
Nimefika Singida, Tabora, Mbeya, Nachingwea, Masasi, Kilwa zote, Lindi, Nanyumbu, Newala, Tandahimba na kijiji kimoja kinaitwa Kitaya Mtwara Vijijini.
Dar es Salaam yote nimeivuruga. Professionally nimekuwa sales manager hapa Dar so najua chocho nyingi hadi nje ya mji kama Zingiziwa huko. Nishafika hadi Pemba Mnazi Kigamboni. Kiufupi hakuna sehemu siijui hapa DSM.......kuna barabara 1 tu sijawahi kupita. Kutoka Madale kupitia Mbopo kwenda Mabwepande.

Nimefika Tanga, Kilimanjaro, Arusha hadi Babati na Kondoa, Mbulu hadi Karatu.
Sehemu ambazo sijawahi kufika kabisa ni mkoa wote wa Songwe, Rukwa na Katavi, Kigoma na Kagera, Pemba na Songea mjini. Tunduru nilifika.

Tofauti na huku ukanda wa Pwani, nipeleke tu Mwanza kaniache, kanda ya ziwa Yaani Geita, Kahama, Mwanza comes first of all.
Reasons:
1. The people......The Sukuma are friendly, above all the city has a mixture of people of diff tribes making it a small Dar. The Haya, the Ha, Chagga, Kurya and the local Sukuma make the most business people in the city without forgetting Hindus and Arabs.

2. The economy......Mwanza is more or less like Dar in almost everything.
3. The weather....moderate temps just like Dar

I love Mwanza.
 

Wanawake wa kimwera pasua kichwa sana…Utasikia m huyu kaka “nimemghaili”…..Na wanapenda sana mgawane mali
 
Mkuu maswali gani hayo kila Veta haikosi vimwali
Kaka nakata tiketi kesho. Naondoka Mtwara jumapili asubuhi nalala mtwara jumapili jumatatu naripoti nakuweka logistics zangu then nikiwa narudi Dar nitakaa Lindi kama siku 3 then narudi Dar halafu mwezi wa pili ndo narudi Mtwara rasmi. Nitakuwa nakuja sana Lindi. Pia nitatembelea kote Nachingwea Masasi Newala Ruangwa Liwale Runduru etc labda kasoro Kilwa tu
 
Ee bwana ee mie roho ilitua Tanga, kamji flani hivi kako kwenye strategic position, nikitaka kuja dar kwenye michongo ni chap nikitaka kwenda arusha ni chap, hali ya hewa si joto si baridi, watoto wazuri wamejaa, maisha ni cheap sana sababu ya vyakula vingi, mzunguko wa pesa ndio unachipukia so kwa mm nnae anza maisha ni rahisi kuweka network zangu vzr for my future, sehemu za starehe, beaches, cinema, ni kama dar tu, ma don wapo, bandari ipo, viwanda na ajira kibao, plots cheap, vifaa vya ujenzi cheap, mji umepangika hau boi, hakuna foleni mjini, barabara moja ikijaa chap una shift kwenda nyingine maisha yanasonga.... anyway labda kama kuna wa kuongezea
 
Ko uko hapo mbamba bay unafaidi kutazama miili ya mabinti wa watu?
 
Kijiji gani lindi kuna mabaki ya waarabu?
Ukiacha hapo town?
Sijajua kilwa pia!..
Wasalimie lindi hasa watu wa kitunda.
 
Mimi Tanga 😅😅😅kwanza maendeleo yanakuja kwa kasi ,fursa nyingi sana ...Watu wanajielewa maisha rahisi kila unachojua Tanga kipo ....Nyongeza kuna soda za huku zinaitwa Healtho kama juisi ,kuna Tangastone kwa kupambania nyumba zinabamba sana ...Cement bei ya kawaida .
 
Sumbawanga hasa pembezoni kama Tamasenga,Kihanda,Mpui,Miangalua, na Laela.
Laela ipo pembezoni kwani!! Si road kabisa ama!!
Sumbawanga yote poa tu sema baridi baadhi ya sehem ndo mtihani..
Ila kalambo nkasi fresh tu..mpaka ulumi kule.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu yan Dom, Iringa na mbeya imechangamka? Au umekosea kuandika?
Dom iringa bado hazijachangamka.
Iringa pazuri kwa uoto asilia.
Dodoma tatizo la ukame ni mtihani sanaa
Ila mbeleni nadhani patakujachangamka vibaya mno maana mabadiliko yanaongezeka mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…