Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Muelekeze hapo akipanda gari ashuke mizani ya zamani kibaha konda yoyote ukimuambia nishushe hospitali ya macho wanajuwa kituo.Mkuu nimewapata kumbe wanaitwa WIPAHS
Ukishuka bodaboda buku tu, ukifika hapo hospitali registration na vipimo haizidi elfu 20, ukikutwa una cataract mtoto wa jicho unapewa appointment siku ya kuja kulazwa na kufanyiwa surgery bure gharama zinalipiwa na wafadhili, chakula bure na miwani bure na dawa bure.
Daktari Umbaro ni daktari bingwa wa Macho ametokea Ndanda mission kwa Wajerumani kwahiyo wana daktari bingwa wa kuaminika.