Uchaguzi 2020 Nipeni miaka mitano muone maajabu

Uchaguzi 2020 Nipeni miaka mitano muone maajabu

Nasikitika sana siamini kama hizi makitu zinatoka kwako arif.
Mkuu tuikubali demokrasia kuanzia kwa mtu mmoja mmoja. Hii ndiyo demokrasia na political tolerance yake.

Usinishangae ukinishangaa unaniambia nami nikushangae. Mwisho wake utakuwa sio mzuri.
 
Mwaka 2015 ulipewa miaka mitano na kwa kweli tumeona maajabu mengi.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu watumishi wa umma wakasota miaka mitano bila kupata nyongeza ya mshahara ambayo ni haki yao kisheria. Gharama za maisha zikapanda lakini kipato cha watumishi kikabaki kilekile. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia wahitimu wa kada muhimu kama udaktari na ualimu wakisota mtaani bila ajira lakini hospitali hazina madaktari na shule hazina waalimu. MAAJABU.

Tukashuhudia watu wa Kimara wakivunjiwa nyumba bila kulipwa fidia kwa kutumia sheria ya kikoloni ya mwaka 1932. Wakaenda mahakamani, na mahakama ikaweka zuio, lakini amri ya mahakama ikapuzwa na nyumba zikavunjwa. MAAJABU.

Tukashuhudia bunge likifanyiwa "shooting" kama bongo movie. Hotuba za wabunge zinakua censored kwanza. Walioongea maneno makali wanakatwa, walioipamba serikali wanaenda hewani. Bunge likapoteza focus na kuanza kuipongeza serikali wakati kazi ya bunge ni kuisimamia serikali. MAAJABU.

Tukashuhudia RC akivamia studio na mitutu ya bunduki kulazimisha "clip yake ya umbea" irushwe hewani. Chombo husika kikaamua kuzingatia maadili na kukataa kurusha clip hiyo. Waandishi wakavamiwa na kutishwa. Waziri aliyeunda Kamati ya kuchunguza suala hilo akafurushwa. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza mifuko ya hifadhi ya jamii ikafuta fao la kujitoa. Watumishi wa mikataba na wa muda mfupi wakaambiwa hadi miaka 60. Mtu mwenye akiba ya 5M na kwa sasa ana maika 25 unamwambia hadi afikishe miaka 60? Yani miaka 35 ijayo? Akifikisha miaka 60 hiyo 5M si itakua ya kununulia mkate tu? MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia Hakimu aliyekua kwenye likizo ya kustaafu akiteuliwa kuwa Jaji wa mahakama kuu. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia mbunge akipigwa risasi kwenye makazi yenye CCTV camera. Lissu akasema camera ziliondolewa baada ya tukio. Hakuna mshukiwa hata mmoja aliyekamatwa hadi sasa. MAAJABU.

Tukashuhudia mikutano ya siasa ikipigwa marufuku kinyume na katiba na sheria za nchi. Viongozi wa upinzani walipofanya vikao vya ndani walikamatwa lakini CCM walifanya mikutano ya hadhara na vikao bila bughudha. MAAJABU.

Binafsi naona maajabu yametosha baba. Hatutaki maajabu mengine.!

Malisa GJ
Hakuna maajabu yoyote jiwe anaweza kufanya zaidi ya kupoteza watu katika mazingira ya kutatanisha.
 
Mkuu tuikubali demokrasia kuanzia kwa mtu mmoja mmoja. Hii ndiyo demokrasia na political tolerance yake.

Usinishangae ukinishangaa unaniambia nami nikishangae. Mwisho wake utakuwa sio mzuri.
1.Political tolerance, Yes!!
2.Demokrasia hell no!!

Kila la kheri. Btw uko bongo land au kule kwa siku zile?
 
Mkuki siku zote kwa nguruwe lakini si kwa binadamu! Halafu unaandika ujinga ujinga wako. Kwa vile waliodhalilishwa hawakuhusu!
......
 
Kwa nini EU na merekani na inchi zingine za ulaya mabalozii wao hawatoi matamko tena kuwaonya chadema na act wazalendo juu ya kufunya mikutano yenye misururu ya watu kwa kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa korona?
Mbona wako kimya saanaa?
Au nawao wanaamini Tanzania hamna korona kama magufuli ambavyo anaamini??
Jana mlisema Dodoma hakuna nyomi, leo
Mnaifufua ile corona mliyo izika! Mmeshikwa kunako ubaya, mtaweweseka sana!
 
Kama rais ni mtu sio Mungu kwani ni lazima uyo mtu awe Jpm?.Isitoshe kama ni kua raisi tayari kashakua kwahiyo anaweza akapatikana mwingine na nchi ikaenda vile vile.
Asante...

Hatutakuja kupata kiongozi Mungu.

Ila wapinzani waache wapnge maana kupinga ndiyo uhai wao. Waendelee tu.

Kipindi cha Mkapa walilalamika Rais dikteta hafai kututawala.

Akaja JK tukamsema huyu kageuza nchu shamba la bibi. Tu/wakatamani kiongozi mwenye mamlaka. Anayeweza kunguruma kidogo.

Akaja JPM...malalamiko hayajaisha. Rais ni mtu sio Mungu. Lazima wawepo wa kuumizwa na wa kufurahishwa na maamuzi anayotoa.
 
Kama rais ni mtu sio Mungu kwani ni lazima uyo mtu awe Jpm?.Isitoshe kama ni kua raisi tayari kashakua kwahiyo anaweza akapatikana mwingine na nchi ikaenda vile vile.
Ndiyo maana wagombea wapo wengi mkuu zaidi ya watano.

Kinachofanyika tarehe 28 0ctoba kila mmoja anaenda kumchagua wake.

Atakaechaguliwa na wengi anatuongoza. Sina shida kabisa na atakayeshinda tofauti na JPM.
 
Wanafunzi wa Yesu na watu waliokua wanamfuata kujifunza kuna siku walishikwa na njaa.

Walipomfuata Yesu kuwa wana njaa wanahitaji Chakula ,Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye Juu ya Yote na mfalme wa wafalme aliwapa chakula.

Cha ajabu kabisa Mwana wa Mungu aliyejua mahitaji makubwa ya binadamu hakuwapa Reli au Daraja au Majengo ya maofisi.

Wana wa Israel kuna wakati walipokuwa jangwani walikosa Chakula Mungu muumba wa vyote aliwapa Mana lakini hakuwanunulia ndege ya kuwahi kufika Kaanani. Alitaka kuwajengea misingi ya kumjua Mungu na kuzishika amri zake kwa Haki.
Haki inapotafutwa pale ilipokosekana ina gharama kubwa sana mana Mungu hapendezwi na hofu inayowafanya wanadamu kufanya uovu dhidi ya wengine.

CCM na viongozi wa dini ambao ni makada wa CCM wanaoiona CCM kama dhehebu la dini wajue wazi kabisa kuwa bila Haki kusimama kwenye Taifa hili amani itakua ni ya muda sana. Majengo ,mareli ,madaraka makubwa,misafara ya kifahari,kugawa mapesa majukwaani,kutoa masadaka ya kujenga makanisa na misikiti haitasaidia mana hata Gadaf na Sadamu walifanya makubwa sana na kujenga nyumba za ibada lakini Chuku haikutoka kwa wale waliogandamizwa na kufanywa daraja la kukanyaga kwenda juu ili hali wenzao wakiwaona kama takataka naawazo yao kuonekana kama ya kijinga yasiyofaa alimradi wao watulie tu watapewa chakula kama kuku wa kisasa na sio binadam. Mungu haoni shida kuruhusu jambo lolote kuinuka juu ya nchi na wanadam wasiotenda haki.

Wenye madaraka wanajipenda wao sana na ndio maana wanaona sifa kuamuru majeshi kuwaangamiza wengine huku wao wakijilinda kwa kila aina ya ulinzi.

Labda tuwakumbushe CCM na viongozi wa Dini maelekezo ya Mungu wa Haki ni kuwa kila Mtu ampende jirani yake kama nafsi yake.
Na kile usichopenda kutendewa usimtendee mwenzako.

Tukiyapuuza haya na kuipigania CCM ili ishinde wale wenye madaraka wajihakikishie kuendelea na madaraka na Teuzi zao huku wao wakiwatendea mabaya Wapinzani wao hakika hata Mungu hawezi kukaa kimya. Hata shetani hatakaa kimya mana ndiyo furaha yake itatimia huku Mungu akihuzunika kwa mabaya yanayotendeka.

Kwa Muda Mrefu tumeibiwa na CCM kwa sababu ya kupuuza haki na sheria.
Mikataba mingi mibovu imetokana na kupuuza sheria na kutoisoma kwa umakini.
Ni Yeye Lisu aliyesema wakati wezi wanaiba. Wengine walikaa kimya tukaibiwa wakisubiri zamu yao nao waibe kwa mbinu mbaya zaidi ya kuwanyamazisha watchdog.
 
Back
Top Bottom