Upwork kumekuwa na kazi nyingi za ku upload app google play store. Unakuta mteja anatoa mpaka $10 per app.
Mteja huyo unakuta ana app zaidi ya 3 sasa kwa hesabu ya kawaida $10 × 3 = $30. Na mteja huyu maswala ya documentation zote anafanya mwenyewe.
Google play console account ni $25, maswali yangu ni Kwa nini mtu atumie pesa nyingi ku upload app kupitia account za wengine na asilipie account yake mwenyewe kusudi awe na full access.
Wengi wa wateja hawa ni Wahindi japo na nchi zingine wapo lakini wahindi ndio wengi.
Wakuu mwaweza kuwa mnajua sababu za wao kutumia account za wengine badala ya za kwako.
Point ya pesa ya kulipia account siihitaji.