Hili ni common sana. Nimeshaona mwanamke akishuka kwenye dala dala mtu akamwambia alikuwa amekalia makohozi, akasema mbona nilikuwa sijakaa kabisa nilikuwa nimesimama. Akaambiwa jiangalie kwenye makalio! ...... alichokiona!!
Haya mambo yanatokea kila siku kwenye dala dala. Yaani ni kila siku. Nimeshaona zaidi ya mara tatu mtu akikurupushwa! Kuna kesi ilishawahi kutokea miaka ya nyuma kidogo kwenye foleni, sujui ilikuwa benki, tena huyo mwanaume alikuwa Daktari wa Mifugo ..... Wataalam waliita mfadhaiko.
Ila inaonekana ni hali (mfadhaiko) inawapata wanume wengi wanapokuwa kwenye mgusano wa kimwili (physical contact) na wanawake kwa muda mrefu. Wengine huamua kujichafua wenyewe ndani ya masuruali yao, wengine huuchomoa kabisa!!! Ila kunakuwa na matatizo ya kisaikolojia, ndo maana wataalam wa akili wanasema binadamu wote ni vichaa ..... tunatofautiana viwango tu!
Ila jambo moja lililo wazi, kuna wanawake wanajisahau mno, yaani hajijali. Mwili wa mwanamke unatakiwa usitiriwe vizuri kuepuka mambo kama haya. Kwenye madaladala kuna wanawake wengine unakuta almost kakumbatiwa kabisa na mtu ambaye hata hamfaham ila yeye unakuta tu katulia na wala hajali. Wanawake wengine unakuta amemsukumia kifua mwanaume kwa muda mrefu wala hajali. Hili ni tatizo, mguso wa kifua cha mwanamke ukiwa mrefu sana kwa mwanaume, hata kama hakuwa na wazo, MFADHAIKO HUWEZA KUTOKEA. Wanawake wengine wanafanya maksudi kabisa kwa nia ya kumuumbua mwanaume. Kwenye dala dala kuna vituko, we acha tu. Ukisimuliwa matukio yaliyotokea kwa siku moja tu huna hamu.
kwa ujumla mwanamke inatakiwa ajiepushe kabisa na mgusano wowote na mwanaume; hasa ikiwa mgusano huo unachukua muda mrefu!! Hata mkikaa kwenye kiti kimoja, si lazima msuguane mabega (hasa kama mwanamke amevaa nguo inayoyaacha wazi)!!
Wanawake wengine hawataki hata kutumia magari ya binafsi kwani wanafurahia wanapobambwa bambwa kwenye misongamano ya kwenye madala dala - atalalamika tu akiibiwa cheni yake, ila mengine poa tu. Haya ni matatizo yaliyopo kwenye jamii, hadi yanapokukumba ndo unastuka; ila yapo kwa sana tu!!