Nipo Buza, nipande Magari yapi nifike Mwenge?

Nipo Buza, nipande Magari yapi nifike Mwenge?

Panda za Makumbusho au Kawe...
NB: Za kawe Zitakurahisishia zaidi kwa sababu utapanda gari moja tu.
 
Sawa mjumbe wa Kyela naona umekuja likizo kidogo kurefresh
 
Route yoyote anafika kaka...japo route ya kupitia Mandela road- (Ubungo) itakuwa rahisi zaidi kwa sababu mzunguko wake sio mrefu kama zile zinazopitia Magomeni.
Kwa njia ya Mandela Road inabidi apande gari ya Temeke-Mbezi yenye ufito wa njano na kijani ndio zinapita Ubungo.

Akishuka Ubungo kule Darajani itabidi apande gari za T/Segerea-Kawe au G/Mboto-Makumbusho ili ashuke Mwenge.

Hii njia si sahihi kumbuka kakwambia anatoka Buza, hivyo atalazimka kupanda gari 3. Apande gari ya Buza ili aende Temeke kisha aendelee na safari, huku ni hasara atatumia muda mwingi na gharama.
 
Panda za Makumbusho au Kawe...
NB: Za kawe Zitakurahisishia zaidi kwa sababu utapanda gari moja tu.
Kumbe route ya gari moja IPO?? Mana nataka nianze kusoma British school center IPO uko mwenge,, SAS nikiwaza gari mbili kwenda na kurudi yan itakuwa balaa sana
 
Duh
Kutoka Buza kwenda Kawe lazima upande gari 2.
Panda gari ya Buza-Makumbusho ukifika Makumbusho uchukue gari yoyote ya kupita Mwenge iwe ni za kwenda Bunju/Tegeta/Mbezi au Mawasiliano(Simu 2000) kisha uwaambie wakushushe Mwenge.

Bon Voyage
Duh kumbe gari mbili??
Asante kwa muongozo wako kiongozi
 
Back
Top Bottom