Nipo chuo kikuu ( MZUMBE ) Morogoro; Naombeni msaada kwa moyo mmoja

Nipo chuo kikuu ( MZUMBE ) Morogoro; Naombeni msaada kwa moyo mmoja

diet

Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
56
Reaction score
8
Mimi ni mwanachuo mwaka wa kwanza Mzumbe, kama mjuavyo chuoni kuna presentation za hapa na pale. Tatizo linalonikabili ni kushindwa kabisa kuongea ninapofika pale mbele ya darasa, nasika kutetemeka, roho inakwenda mbio sana,midomo inakauka kabisa yaani naskia kuanguka.

Nimejaribu kufata jinsi wenzangu wanavyonishauri ili niweze kushinda hali hiyo ila nimeshindwa kabisa hivyo naongea kidogo tu nashindwa kabisa kuendelea kwani sauti inatoweka kabisa nashindwa kuongea. Naskia uchungu kuona wenzangu wanavyoongea vizuri mbele ya darasa lakini mi nashindwa kabisa.Kwa mwanafunzi yeyote atakayekuwa yuko na mimi kozi moja na darasa moja hope atakuwa amenijua hivyo naomba pia anipe ushauri kama bado hajawahi kunipa tukiwa group discussion.

Mwisho wanaJF wote natumai mtanipa ushauri utakaoweza kunisaidia.
 
yeah,,,,,,,,niko nondo mbaya na si kwamba najifagilia kwani hata kwenye group wananipenda cose nikiwa na group sina shida kuongea na kutoa maelezo,,,,,,tatizo tu nikiwa mbele ya darasa ndio ishu,,,,,,,,,nasahau kila kitu nilichopanga kuongea
 
We dogo sikiliza huo woga wa kuongea kila mtu huwa anao.Hata mimi nilikuwa hivyohivyo tena afadhari ya wewe ila kwa sasa niko fit baada ya kugundua tatizo linakuwa wapi.Woga wa kuongea mbele za watu hudumu kwa dakika 3 tu,baada ya hapo unakuwa unaona kama unaongea na watoto wadogo.Kosa unalofanya ni kukaa dakika 2 pale mbele na kuondoka,ukiendelea hivyo woga hautaisha kaa muda kidogo kwani dk 3 za kwanza ndio huwa zinatetemesha watu.
 
zaidi pia tangu niko shule chekechea hadi hapa nilipofika sijawahi kabisa kufanya presentation sababu mi nimesoma msingi kijijini na secondary pia kijijini,,,,,,,,,,,,ila five na sx kidogo ndio ilikuwa mjini sababu shule ilikuwa wilayani.....huko kusini huko,,,,,, sasa hivi ndio niko morogoro yaani nimekutana na presentation nashindwa kabisa kuongea,,,,,,,ila moyoni naumia sana ninaposhindwa sababu najitahidi lakini wapi,,,kuna rafiki yangu kaninunulia vitabu viwili nimevisoma lakini wapi,,,,,,vyote ni vya public speaking, pia nimesoma sana kupitia internet jinsi yakuweza kuongea mbele za watu lakin badi haijanisaidia,,,,,,, yaani siku ya presentation naiwaza,,,,,,yaani km ni kesho usiku silali,nakuwa nawaza na kushtuka jinsi ya kwenda kuongea pale mbele,,,,,,,yaani jamani mwenzenu napata tabu si siri,,,,,nisaidieni jamani
 
huwa ninavyozidi kukaa ndio nashindwa kabisa,,,,,,,,,,,naskia kuanguka,,,,,,,,,,,hiyo pia waliniambia wenzangu kuwa unavyozidi kukaa pale mbele ndio unazoea na hali hiyo inaisha unaendelea kuongea lakin kwangu ni tofauti utanionea huruma
 
una tatizo la woga wewe, kinachotakiwa ni kuwashusha wanafunzi wote walio mbele yako na kuwaona wasio na uwezo zaidi yako kitaaluma, pili, usiogope kuwaangalia we wakazie macho tu, tatu, epuka mtindo wa kusoma each and every thing kwenye karatasi wakati wa kupresent kwa kua utakua unakosea kosea kwa hofu. kinachotakiwa usome hoja then ielezee kwa lugha yako ukiwa umetulia hope utajijengea ujasiri
mwisho, hutakiwi kuiwaza waza presentation iliyo mbele yako mara kwa mara, jifanye unaipotezea moyo hautodunda kwa hofu. ukiwa mbele yao kama wasiwasi na kutetemeka kunaendelea basi usisimame sehemu moja muda wote, jaribu kuzunguka hapa na pale huku unapresent pale mbele
 
Usiwatazame watu usoni. Watazame juu ya vichwa vyao (utosini). Wao wataona kama unawaona kumbe wewe unakuwa haumwoni mtu huku ukiendelea kumwaga matirio. Njia hiyo nimeitumia sana na ilinisaidia sana mpaka nikawa mzoefu. Nategemea kukuona siku moja ukiwahutubia wananchi wakuchague kuwa mbuge au rais. Kila la heri.
 
unakunywa pombe? confidence inauzwa kwenye bia, am kidding, JIPE MOYO WE NI MWANAUME, HUWA UNTONGOZAJE?
 
punguza kupata diet kama manyama nyama,machps..etc, kama Id yako.
 
Yawezekana tatizo likawa ni lugha.Usiombe king'eng'e kikwame.Utasikia me....you....I mean,the...this.Jifue kilugha tu usonge mbele
 
Waone wenzio kama nyau tu ndo maana wengne wanakula ndumu na konyagi alafu wanaenda kupresent.
 
Pole sana, Its a common psychological problem(stage fright, na unahitaji matibabu na kufundiswa skills za kufanya presentation. Sijui kama Morogoro kama kuna psychologists wanaoweza kukusaidia, ila kwa Dar, najua wako wengi kidogo, hata ukienda Muhimbili.

Na kwa wale wote mnotumia ndumu , ulevi ili kucope, kiukweli mnaogezea tatizo, tafuteni tiba ipo kwa hofu zote.
 
yeah,,,,,,,,niko nondo mbaya na si kwamba najifagilia kwani hata kwenye group wananipenda cose nikiwa na group sina shida kuongea na kutoa maelezo,,,,,,tatizo tu nikiwa mbele ya darasa ndio ishu,,,,,,,,,nasahau kila kitu nilichopanga kuongea
na lugha unayotakiwa kutumia je inapanda? maana kwa wote tuliosoma Bongo tunajua huko kwenye ma-group discussion tunaongea kuswahili mara nyingi. sasa inapokuja darasani unatakiwa kuongea kizungu..... inakuwaje hapo?
 
We ukifika mbele ya darasa gonga kienglish, ukifika mahali ukiona unakwama unaingiza na lugha yako ya kinyumbani ili kuwachanganya zaidi, wakati wanafikilia ulikuwa unaongea nini mzee unakuwa tayari unamalizia. Ni maujanja tu na kuwa na uso wa mbuzi mbele za watu, Usicheke na mtu. Unaogopa nini kwani ukikosea unapelekwa mahakamani!!!!. Wewe payuka tu ili mradi uelewe unachoongea.
 
Kuna dem ume mzimia wewe sasa we baada ya kutiririka nondo we bichwa lime zunguukwa na vikopa kopa tu lazima utoe GUKOPA!!!
 
Maranyingi lugha ndio chanzo cha kutojiamini. Ila jipe confidence ukae kwa muda kidogo hapo mbele kama alivoshauri Jamaa hapo juu, pia ukipresent usitizame mtu mmoja mmoja usoni! Unaeza kuta anacheka ukajua anakucheka! Pia hiyo documents usiishike mkononi maana ukivibrate na karatasi zinavibrate zaidi. Tafuta meza then weka docs juu ndio usome. Hii kitu ya kushika karatasi mkononi imewaumbua wengi sana na Mimi nikiwemo!
 
Waone wenzio kama nyau tu ndo maana wengne wanakula ndumu na konyagi alafu wanaenda kupresent.
kwa nini ulewe ndo upresent? kama material unayajua na lugha ya kupresentia inapanda una haja ya konyagi kweli? sasa hiyo itakuwa presentation ya shule au wosia kwa maharusi?
 
Back
Top Bottom