Nipo Dar, biashara ipi inalipa kati ya kukaanga miguu ya kuku na kukaanga mihogo?

We si unaona mleta mada ndio anaanza kujitafuta SA vijana atawalipa Nini!
Hua tunatumia mfumo wa posho baada ya kufunga kazi, Kwa mfano kila siku akianza na kijana mmoja walau akiwa anampa 5000 kila baada ya kufunga kazi sio mbaya na baadae ataongeza mwingine Kwa ajili ya kurahisisha kazi pale itapokua biashara imekua, Hata makabati anaweza asimudu alminium akatengeneza ya kioo lakini pembeni mbao Kwa kuanzia
 
Unaweza niambia kilichokufurahisha hata na mm napenda kufurahi😁
Mtaani kwako ulishaona muuza miogo au miguu kaajiri "vijana"!?
Hizi ni biashara za kuanzia ambazo ni ngumu sana kuweka vijana
Mchangia hoja kawaza pakubwa sana
Anyway furaha hutegemea na mtu
 
Nimejikwaa kidogo mkuu ulikuwa utani tu
 
mkuu Kuna vijana Wana lipwa 3000 saidia chipsi, so hata yeye ana weza tafuta wa hivyo.
 
Mtaani kwako ulishaona muuza miogo au miguu kaajiri "vijana"!?
Hizi ni biashara za kuanzia ambazo ni ngumu sana kuweka vijana
Mchangia hoja kawaza pakubwa sana
Anyway furaha hutegemea na mtu
Ndio baadhi ya wauza mihongo wanakuwa na msaidizi Mmoja tu ila sio necessary
Hata wauza kuku naonaga wapo zaidi ya Mmoja
 
Hapa location iwe Kali sana labda coco beach anyway ni ushauri mzuri
 
Ndio baadhi ya wauza mihongo wanakuwa na msaidizi Mmoja tu ila sio necessary
Hata wauza kuku naonaga wapo zaidi ya Mmoja
Yah kuku na chips msaidizi ni lazima ila mihogo labda kule Coco ila wengi hufanya wenyewe na wale wa miguu ya kuku
 
Yah kuku na chips msaidizi ni lazima ila mihogo labda kule Coco ila wengi hufanya wenyewe na wale wa miguu ya kuku
Hapa nitafute tu dalali ndo ntapata location nzuri ila Mimi nimeshindwa naona sehemu zote nazopita zina watu aisee
 
Hapa nitafute tu dalali ndo ntapata location nzuri ila Mimi nimeshindwa naona sehemu zote nazopita zina watu aisee
Dalali tena rafiki??, uliona sehemu haina watu ujue pame lala mno.

we fungua sehemu Kisha boresha huduma tu, mihogo upige rangi ya njano.
 
Hizo biashara hua zinapesa sana sema watu huzidharau bila ya kujua
Yah ukipata location nzuri na ukajua mapishi zinalipa vizuri wateja wakubwa ni wanafunzi na watu wa mtaani ila kikubwa huwa hazibebwi na usafi sana Bali mapishi
Hapa mtaani Kuna mama ye ameweka vizuri kwenye dell na kameza kazuri mwenzake anauzia jikoni na kwenye karai lake na watu wanakaa wanangoja
 
mapishi yaani kule juu nilisema taste Kwa mfano mihogo anamenya, anachemsha inakua laini halafu atie kwenye mafuta, kwenye miguu ya kuku na mazaga yote kule taste pia na viungoviungo ili bando zile ziwe na ladha safi, location anaweza kuwaza mbezi louis upande wa daladala, riverside, buguruni darajani, uhasibu mitaa hiyo, zakheim hadi rangi tatu, chamazi na mbande mwisho, maili moja kibaha, kimara darajani hadi korogwe, anaweza suvey barabara ya korogwe pale kama unaenda maji chumvi, hadi kutokea external, akivuka pale barabara aangalie mabibo imekaaje aangalie kigogo ruhanga huko, akizunguka huko atajua wapi aweke kambi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…