Nipo hatua ya kupaua, nijuzeni bei ya vifaa hivi kwa Dar

Nipo hatua ya kupaua, nijuzeni bei ya vifaa hivi kwa Dar

Nyumba ya vyumba vingapi hii

Je Imegharimu kiasi gani mpaka hapo?

Sent from my P00C using JamiiForums mobile app
 
Hongera kwa kumaliza hatua hii ngumu,ulitumia bati ngapi 140 kama ulivyofanyiwa makadirio au zilipungua?
Hapana mkuu,
Nilikomaa sana,
Nikatumia bati 106.

Nilichukua miongozo mingi ya wadau iliyotolewa kwenye huu uzi,
Ikiwemo kupunguza idadi ya vitu.

Kwa mahesabu ya awali ya fundi, ilifika Sh. 7,962,000/-,
Ila nilipozingatia maoni ya humu, plus kusimamia zoezi Mimi mwenyewe, nimekamilisha kwa Sh. 5,358,500/-,

Hivyo nimeokoa kiasi Cha Sh. 2,575,500/-, ambayo nimeipeleka kwenye bajeti ya grill (madirisha na milango).

Kama tuna nafasi, tukubali kupigwa jua kwa kushinda saiti na mafundi kwa siku kadhaa ili kukamilisha zoezi fulani, inasaidia kuokoa hela nyingi.
 
Ukifika kipande cha kuweka tiles nichek nikupe tiles kali..
Contact:
0744928908
IMG_20220112_165932.jpg
 
Mkuu,
Fundi nd'o ameniandikia hivyo,
Sijapunguza wala kuongeza chochote.

Kwa kuwa huu nd'o ujenzi wangu wa kwanza,
Naomba unielimishe ambapo kuna utofauti mkubwa ili nisije kupata hasara.
Mkuu, ukisema bei za Dar, Dar kubwa sana. Kama upo mjini, nakushauri tembelea madukani wewe mwenyewe, usitafute majibu humu. Wengine wapo kwa Mtogole, wengine wapo Sinza nk. Rahisisha maisha, kama umeweza kujenga hadi hatua ya kupaua huwezi kushindwa kujua bei za hivyo vitu, mfano mbao na nondo, hivyo si umevitumia wakati unaweza LENTA!?
 
Mkuu, taja eneo ulipo,
Size ya tiles na bei zake ili tuhamasike kufanya manunuzi kwako au vinginevyo.
Mkuu napatika chalinze
Tiles nazo size zote..
Mfano 50*50 zinatembea kuaanzia 39500 mpk 36000
40*40 zinaanza 30000 mpk 26000
Karibu mkuu
0744928908

IMG_20220313_151654.jpg
 
Mkuu, ukisema bei za Dar, Dar kubwa sana. Kama upo mjini, nakushauri tembelea madukani wewe mwenyewe, usitafute majibu humu. Wengine wapo kwa Mtogole, wengine wapo Sinza nk. Rahisisha maisha, kama umeweza kujenga hadi hatua ya kupaua huwezi kushindwa kujua bei za hivyo vitu, mfano mbao na nondo, hivyo si umevitumia wakati unaweza LENTA!?
Ahsante sana mkuu.
Tayari hatua hii imepita.

Sasa nahangaika na mambo ya wiring, blundering, plasta, skimming n.k.
 
Mkuu,
Kwa makisio haya uliyonipa,
Nitajitahidi kusimamia mwenyewe zoezi lote.
Hata chakula nitaagiza niletewe hapohaoi saiti.
Afadhali usimamie mwenyewe mkuu.japo wakati mwingine mafundi wanaweza kukupiga nawewe ukiwa hapo hapo! mimi nilikuwa najenga na nikampa jamaa yangu anisimamie huo ujenzi..baadae majirani wale site wakamwambia mke wangu " yaani ninyi hadi mnamaliza kujenga, na huyo jamaa yenu kamaliza nyumba yake!"...ilibidi nijiongeze mkuu!
 
Back
Top Bottom