Nipo kanisani, huyu Askofu kila mada anayotoa leo naona ananilenga mimi, nikipata nafasi nachomoka hapa

Nipo kanisani, huyu Askofu kila mada anayotoa leo naona ananilenga mimi, nikipata nafasi nachomoka hapa

Kevzy

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2026
Posts
976
Reaction score
1,712
Kwanza sadaka sitoi

Huyu bwanah anatoa maandiko huku ananikodolea macho nafikiri atakuwa ameelekezwa tu namtu anipige vijembe

Kaanza na mada za ugomvi na kupigana , anazungumza huku ananitolea macho japokuwa nimekaa nyuma ila ananitolea macho mpaka huku alafu ana macho makali kinoma yaani

Akaja na mada ya uzinzi na uasherat automatically hizi mada zinatulenga sisi mabachela, na bado anakabia juu tu ananikodolea mimacho , kwanini? Leo ibada anaongoza yeye

Hapa naandika uzi najifanya kama nafatilia maandiko kwenye sim

Sasa hivi anaendelea na mada ya kuwa vijana tunatakiwa tuoe tena tuoe na tusikawie na bado ananikodolea tu macho , nikipata nafasi hapa nachomoka aisee na sirudi tena mpaka jpili ijayo
 
Screenshot_20260802_093628_Google.jpg
 
Back
Top Bottom