Nipo kwenye basi hili lijamaa linasoma mgs zangu nimegeuza kamera nikalinasa

Vieepe yai🙁
 
Mgegede

"the highest risk should give maximum profit"
 
Kuangalia simu haina maana ni kusoma msg tu! huenda huyo mtu alikua kweli anatizama simu yako bali akili yake ilikua mbali akitafakari ugumu wa maisha,
 
Hao wa hivyo wamejaa sana na saa nyingine inakuwa ngumu kuwakataza zaidi ya kuacha unachokifanya na kuweka simu kwenye pochi.

Ila ni tabia mbovu na hata baadhi ya wana jf humu wanayo mana nshawahi ona nyuzi humu mtu anasema ameona mdada member wa jf anaperuzi jf kwenye daladala na kuja kuwasema humu kitu ambacho kinaonyesha kwamba na yeye pia alipiga chabo.
 
Wakuu hili lijitu linasoma msg zangu,
Lenyewe limekosa nafasi ya kukaa badala liangalie miti inavyokimbia nje linaangalia simu yangu, nimfanyeje?


Sent using Jamii Forums mobile app
Ukitaka kujua kama mtu anasoma msg zako unaandika humu ndani nimemuona mtu mmoja wa Kibiti sijui anataka kutufanya nini utaona atakavyokuwa na wasi wasi,unaweza kushangaa akasema yupo wapi huyo mtu.
 
Mpe simu mwambie akusaidie kureply sms since anajua kila kitu.
 
Siku moja jamaa tumekaa naye akawa anachungulia ninavyochati. Ikabidi nijifanye naandika msg nikaandika hivi:

"SAMAHANI BABU HUYU NYOKA ULIYENITUMA NIMEMWEKA MFUKONI SASA NAONA ANANITEKENYA ANATAKA KUTOKA, VP HATAWADHURU WATU?"

Jamaa hapo hapo akasimama anaanza kunichungulia mi nikaweka simu mfukoni.

Nikatulia nikawa najifanya nampanga vizuri nyoka, jamaa alifika safari yake hana amani kabisa nadhani alienda kusimulia mkewe
 

Dar wapi daladala inapita barabara ina miti mingi pembezoni?
 
Sasa mkuu kama huyo unaanzaje kumuuliza wakati wewe umekaa yeye amesimama ,hebu tusaidiane kupeana mbinu basi ambazo kama ni wewe ungezitumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…