Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Tangu nifike Mtwara miezi kadhaa iliyopita, mambo ninayokutana nayo sikuyategemea kabisa. Picha inaanza wakati nakuja kuripoti, ile nafika bus stand ya Mkanaredi naambiwa hapa ndiyo Manispaa ya Mikindani na ndiyo mjini.

Sikuamini! Mr. akanitia moyo na kuniambia nitazoea mazingira. Nikasema, "Sawa, maadam ni mjini, kitu cha msingi ni huduma."


Tukachukua lodge (na lodge zenyewe maji hayatoki, wanategemea maji ya mvua... yani ni tafrani tupu!). To cut a long story short, maisha ya Mtwara ni magumu kwenye nyanja zote! Maji ni shida, bei ya vitu iko juu sana kuliko hata Dar es Salaam, na miundombinu hafifu inafanya usafiri kuwa wa tabu.

Huduma za kifedha ni chache na ziko mbali, yani kulala au kushinda njaa ukiwa na hela mfukoni ni kitu cha kawaida sana hapa!

Ikifika saa 3 usiku, barabarani ni nyeupe kabisa—huoni mtu, na maduka yanafungwa mapema. Viwanja vipo, lakini The Shooters ndicho kiwanja pekee nilichoelewa, na nikiwa hapo najihisi kama niko Dar es Salaam.

Serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa!
Mimi nilipangiwa mamba, moshi vijijini, kabla sijafika huku nilifikiri ninaenda sehemu iliyoendelea kuliko zote Tanzani.. kutokana na sifa za mwana JF, Lwambo Makiadi, kwamba moshi ni kama ulaya.
1. Hakuna maji
2. Hakuna umeme
3. Hakuna mtandao wa simu au internet
4. Barabara ni mbovu kamaza ngombe
5. Hakuna watu...vijana wamelewa muda wote
6. Chakula hakuna
7. Mbunge ni kama hawana
 
Mimi nilipangiwa mamba, moshi vijijini, kabla sijafika huku nilifikiri ninaenda sehemu iliyoendelea kuliko zote Tanzani.. kutokana na sifa za mwana JF, Lwambo Makiadi, kwamba moshi ni kama ulaya.
1. Hakuna maji
2. Hakuna umeme
3. Hakuna mtandao wa simu au internet
4. Barabara ni mbovu kamaza ngombe
5. Hakuna watu...vijana wamelewa muda wote
6. Chakula hakuna
7. Mbunge ni kama hawana
Wanawake pia hakuna au wapo? Wote wanaume?
 
Usafiri wa shida, maji yanategemewa ya mvua??!!!, huu ni uongo uliotukuka. Ntwala hapana mvuto tu ila hayo mengine we ntoto umetuongopea
 
Sasa kama watu wa mtwara hawafanyi kazi wanapataje mahitaji yao? Kati ya mtwara na kanda ya ziwa wapi kuliko na watu wengi wanaoishi maisha magumu sana?
Umasikini wa Mikoa ya kusini unaweza kufananisha na kanda ya Ziwa ? kwa wastani kila familia kanda ya ziwa inamiliki ng'ombe 10 tofautisha na wanaomiliki ng'ombe 50,100,500 hadi 5000 kila kaya kanda ya ziwa hukosi Ox Plough mbili hadi tatu kwa hiyo nguvu kazi ya kilimo ni kubwa sn maeneo hayo hata huo mchele mnaokula huko sehemu kubwa unalimwa kanda za ziwa iwe Morogoro na wasukuma hao hao..
 
Back
Top Bottom