Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Tangu nifike Mtwara miezi kadhaa iliyopita, mambo ninayokutana nayo sikuyategemea kabisa. Picha inaanza wakati nakuja kuripoti, ile nafika bus stand ya Mkanaredi naambiwa hapa ndiyo Manispaa ya Mikindani na ndiyo mjini.

Sikuamini! Mr. akanitia moyo na kuniambia nitazoea mazingira. Nikasema, "Sawa, maadam ni mjini, kitu cha msingi ni huduma."


Tukachukua lodge (na lodge zenyewe maji hayatoki, wanategemea maji ya mvua... yani ni tafrani tupu!). To cut a long story short, maisha ya Mtwara ni magumu kwenye nyanja zote! Maji ni shida, bei ya vitu iko juu sana kuliko hata Dar es Salaam, na miundombinu hafifu inafanya usafiri kuwa wa tabu.

Huduma za kifedha ni chache na ziko mbali, yani kulala au kushinda njaa ukiwa na hela mfukoni ni kitu cha kawaida sana hapa!

Ikifika saa 3 usiku, barabarani ni nyeupe kabisa—huoni mtu, na maduka yanafungwa mapema. Viwanja vipo, lakini The Shooters ndicho kiwanja pekee nilichoelewa, na nikiwa hapo najihisi kama niko Dar es Salaam.

Serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa!
mtwara?? we!!
 
Wachq tu wanitusi lakini Huo ndio ukweli
Hawataki kuambiwa ukweli...wanachukia kuambiwa ukweli
Wanaume wa huku wavivu sana! Asubuhi unamkuta barazani kajifunga msuri anasubiri mbaazi zichanue akavune yani hawajishughulishi
 
Noti za huko chakavu!!!

Niliendaga lindi, asee!!! Yaani noti ambayo hata konda wa daladala hapa dar ataikataa kule dukani eti inapokelewa, na chenchi unarudishiwa.

Miji ile sijui watu hawatembei, yaani hela zimechakaa maana yake mzunguko wa hela ni humo humo tu.

Yaani hata ukisimama katikati ya mji wa lindi, ukiamua kurusha jiwe kuelekea upande wowote litadondokea porini.

Yaani kamji kama kiberiti.
Hahaaaa ila we jamaa utakuwa umeongeza chumvi ingawa sijaitembea sana Lindi Manispaa.
Umenikumbusha nilienda Tunduru, nipo katikati ya mji na bado mapori nayaona karibu. Ikabiidi nianze kuwapa story vijana wa pale kuhusu kufuga mbuzi!
 
Hawataki kuambiwa ukweli...wanachukia kuambiwa ukweli
Wanaume wa huku wavivu sana! Asubuhi unamkuta barazani kajifunga msuri anasubiri mbaazi zichanue akavune yani hawajishughulishi
Vibagarashia na mabaibui si ni mengi huko
 
Back
Top Bottom