Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Oky jambo jema brotherNi nzuri mama!
Asante sana brotherSawa mama angu karibu mtwara!
mtwara?? we!!Tangu nifike Mtwara miezi kadhaa iliyopita, mambo ninayokutana nayo sikuyategemea kabisa. Picha inaanza wakati nakuja kuripoti, ile nafika bus stand ya Mkanaredi naambiwa hapa ndiyo Manispaa ya Mikindani na ndiyo mjini.
Sikuamini! Mr. akanitia moyo na kuniambia nitazoea mazingira. Nikasema, "Sawa, maadam ni mjini, kitu cha msingi ni huduma."
Tukachukua lodge (na lodge zenyewe maji hayatoki, wanategemea maji ya mvua... yani ni tafrani tupu!). To cut a long story short, maisha ya Mtwara ni magumu kwenye nyanja zote! Maji ni shida, bei ya vitu iko juu sana kuliko hata Dar es Salaam, na miundombinu hafifu inafanya usafiri kuwa wa tabu.
Huduma za kifedha ni chache na ziko mbali, yani kulala au kushinda njaa ukiwa na hela mfukoni ni kitu cha kawaida sana hapa!
Ikifika saa 3 usiku, barabarani ni nyeupe kabisa—huoni mtu, na maduka yanafungwa mapema. Viwanja vipo, lakini The Shooters ndicho kiwanja pekee nilichoelewa, na nikiwa hapo najihisi kama niko Dar es Salaam.
Serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa!
kwamba mtwara iko nyuma hivyo siku hizi?Nini?
aisee ntakujaNjoo ujionee!
Wachq tu wanitusi lakini Huo ndio ukweli kwingine kwa hovyo walikojazana wavaa kobazi ni Lindi na kigomaNgoja wenye mkoa wao wakusikie uoge matusi🤣
Hahaaaa ila we jamaa utakuwa umeongeza chumvi ingawa sijaitembea sana Lindi Manispaa.Noti za huko chakavu!!!
Niliendaga lindi, asee!!! Yaani noti ambayo hata konda wa daladala hapa dar ataikataa kule dukani eti inapokelewa, na chenchi unarudishiwa.
Miji ile sijui watu hawatembei, yaani hela zimechakaa maana yake mzunguko wa hela ni humo humo tu.
Yaani hata ukisimama katikati ya mji wa lindi, ukiamua kurusha jiwe kuelekea upande wowote litadondokea porini.
Yaani kamji kama kiberiti.
Vibagarashia na mabaibui si ni mengi hukoHawataki kuambiwa ukweli...wanachukia kuambiwa ukweli
Wanaume wa huku wavivu sana! Asubuhi unamkuta barazani kajifunga msuri anasubiri mbaazi zichanue akavune yani hawajishughulishi
unastahili middle finger kabisa weweHuna akili..