Nipo naelekea mahakamani kwenda kutoa ushahidi, kipi cha kuzingatia?

Nipo naelekea mahakamani kwenda kutoa ushahidi, kipi cha kuzingatia?

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,959
Reaction score
24,935
Wanasheria na wazoefu ambao mmewahi fika mahakamani, nimepigiwa simu na mwanasheria wa Serikali niende nikatoe ushahidi.

Kuna tukio lilitokea na mimi ni mmoja kati ya walioshuhudia.

Kipi cha kuzingatia wakati wa kutoa ushahidi.

NB: Nilishatoa maelezo polisi ila leo ndio siku ya kutoa ushahidi mahakamani.
 
Wanasheria na wazoefu ambao mmewahi fika mahakamani, nimepigiwa simu na mwanasheria wa serikari niende nikatoe ushahidi.

Kuna tukio lilitokea na mimi ni mmoja kati ya walioshuhudia.

Kipi cha kuzingatia wakati wa kutoa ushahidi .

NB: Nilishatoa maelezo polisi ila leo ndio siku ya kutoa ushahidi mahakamani.
Kuna scenario moja ilishawahi kutokea miaka ya nyuma, shahidi alijikuta anapigwa dole mahakamani.

Nakushauri vaa jeans mkuu, watuhumiwa wamevurugwa.
 
Zingatia kile ulichokisema kule polisi na unapoulizwa maswali na hakimu au mwanasheria jibu ndio au hapana na sio vinginevyo.

Ukitakiwa kutoa maelezo jinsi tukio lilivyokuwa, anza na siku ya tarehe husika majira unakadiria Kati ya muda flan mpaka muda flan usije ukajiumauma kwani ukigundulika unasema uongo vifungu vya kukushtaki vipo wazi.
 
Zingatia kile ulichokisema kule polis na unapoulizwa maswali na hakimu au mwanasheria jibu ndio au hapana na sio vinginevyo.

Ukitakiwa kutoa maelezo jinsi tukio lilivyokuwa anza na siku ya tarehe husika majira unakadilia Kati ya muda flan mpk muda flan usije ukajiumauma kwani ukigundulika unasema uwongo vifungu vya kukushtaki vipo wazi.
Mahakamani hawajawahi kuyawekea mkazo maelezo ya kutoka polisi kwasababu polisi wetu wanafahamika huwa wanauliza maswali wakati huo wana majibu yao ambayo utake usitake watayaandika.
 
Kuna mmoja Tanga alikwenda kutoa ushahidi, akiwa anajiandaa kutoa ushahidi ghafla alidondoka na kufa pale pale. Mashahidi wengine hawakua tayari kutoa ushahidi.
Kama Ni kesi ya viwanja andika wosia kabisa.
Kufa sio tatizo, nikifa leo yeye atakufa kesho tutatofautiana siku ya maziko tu,
Sikihofii kifo kwa sababu najua kipo na lazima kinikute.

Nb
Sio kesi ya viwanja ni kesi ya vijana wa hovyo wasioweza kufunga zipu zao vizuri ata kwa watoto wadogo.
 
Baada ya kula kiapo Zingatia kusema ukweli tuu ambao uliona kwa macho yako na usije kutoa ushahidi kwa kile ulicho sikia kwa kuambiwa. Kutoa ushahidi wa uongo mahakamani ni kosa chini ya sheria ya kanuni ya adhabu fungu namba 102.

kosa lake ni perjury ukibainika kutoa ushahid wa uongo mahakamani wewe pamoja na mtu aliye kushauri au kukushawishi kutoa ushahidi wa uongo wote mtakuwa mmefanya kosa la
perjury na adhabu yenu itakuwa kifungo cha miaka 7 jela. Kuwa makini mkuu
 
Utaulizwa maswali kuhusu tukio zima. Hakikisha unajibu kulingana na uhalisia wa tukio kwa kifupi kama ulivyoshuhudia bila kuongeza maneno.
Hata kama unajua mengi usiropoke.... Mwendesha mashtaka ndie anayepaswa kukuchambua na kuthibitisha kama wewe ni shahidi wa ukweli.
 
Mahakamani hata Kama kitu kinachekesha husicheke kuwa muwazi na mkweli unachosema usikisahau ukiulizwa Tena utaonekana muongo, hongera kwa kusubutu watu Kama nyinyi tunawataka ktk jamii zetu, mtu kaonewa kwanini uogope kusema ukweli au kutoa ushahidi, usitishike Wala kuwa na mawazo nenda kasimamie ukweli wa haki.
 
Wanasheria na wazoefu ambao mmewahi fika mahakamani, nimepigiwa simu na mwanasheria wa Serikali niende nikatoe ushahidi.

Kuna tukio lilitokea na mimi ni mmoja kati ya walioshuhudia.

Kipi cha kuzingatia wakati wa kutoa ushahidi.

NB: Nilishatoa maelezo polisi ila leo ndio siku ya kutoa ushahidi mahakamani.
Zingatia ushahidi
 
Mahakamani hata Kama kitu kinachekesha husiche, kuwa muwazi na mkweli unachosema usikisahau ukiulizwa Tena utaonekana muongo, hongera kwa kusubutu watu Kama nyinyi tunawataka ktk jamii zetu, mtu kaonewa kwanini uogope kusema ukweli au kutoa ushahidi, usitishike Wala kuwa na mawazo nenda kasimamie ukweli wa haki.
Hapo kwenye kucheka hapo fafanua mkuu kidogo
 
Back
Top Bottom