Nipo naelekea mahakamani kwenda kutoa ushahidi, kipi cha kuzingatia?

Nipo naelekea mahakamani kwenda kutoa ushahidi, kipi cha kuzingatia?

Kufa sio tatizo, nikifa leo yeye atakufa kesho tutatofautiana siku ya maziko tu,
Sikihofii kifo kwa sababu najua kipo na lazima kinikute.

Nb
Sio kesi ya viwanja ni kesi ya vijana wa hovyo wasioweza kufunga zipu zao vizuri ata kwa watoto wadogo.
Kama ya kubaka nenda kaongeze chumviii kabisaaa jamaaa akae nyuma ya nondo swain.....
 
Kuna muda wanauliza maswali ambayo hayahusiani na case ili kukutoa mchezoni.
Hasa vile vizee vya mahakama utadhani kama unachukiwa hivi ila jiamin na ukomae usibadil kaul kila mda
 
Wanasheria na wazoefu ambao mmewahi fika mahakamani, nimepigiwa simu na mwanasheria wa Serikali niende nikatoe ushahidi.

Kuna tukio lilitokea na mimi ni mmoja kati ya walioshuhudia.

Kipi cha kuzingatia wakati wa kutoa ushahidi.

NB: Nilishatoa maelezo polisi ila leo ndio siku ya kutoa ushahidi mahakamani.
Kutoa ushahidi sio kazi nzito cos unaelezea kile ulichoshuhudia tu. Usithubutu kusema uongo maana utahitajika tena uenda leo au siku nyingine kwaajili ya kitu kinaitwa Cross Examination! Hapa kama sio watuhumiwa basi mwanasheria wa upande wa utetezi watachallange ushahidi wako ili kukuvuruga na kuharibu ushahidi wako.

Kuwa mtulivu sana, ikitokea utafanyia Cross Examination siku nyingine basi ni vyema ukiwa na simu yako mfukoni uwe unajirecord kutunza kumbukumbu yako vzr the way uliwasilisha ushahidi ili siku ya Cross Examination wasikutoe kwenye reli.
 
Mahakamani hata Kama kitu kinachekesha husicheke kuwa muwazi na mkweli unachosema usikisahau ukiulizwa Tena utaonekana muongo, hongera kwa kusubutu watu Kama nyinyi tunawataka ktk jamii zetu, mtu kaonewa kwanini uogope kusema ukweli au kutoa ushahidi, usitishike Wala kuwa na mawazo nenda kasimamie ukweli wa haki.
Wangeweka tangazo kubwa kwamba ukiwa mahakami huruhusiwi kucheka.
Wengine hatuwezi kuzuia kicheko😅😅😅
 
Sasa, we hujui kumbe, ndomana kule Kama unajiona huwezi usiende kusikilizaga kesi, wanaruhusu tu watu kwenda kusikiliza.
sio kweli mkuu labda kama vifungu vimebadilishwa juz, coz nimeuzuria kesi aina tano ubakaji, ardhi, madawa, uhujumu, na zote hz watu wanapotolea ushaid kuna vitu vinavunja mbavu unacheka mpakaa ila tu unachek kiutu uzima hahahahaha ikipigwa stop una kata loud unacheka silent
 
Wanasheria na wazoefu ambao mmewahi fika mahakamani, nimepigiwa simu na mwanasheria wa Serikali niende nikatoe ushahidi.

Kuna tukio lilitokea na mimi ni mmoja kati ya walioshuhudia.

Kipi cha kuzingatia wakati wa kutoa ushahidi.

NB: Nilishatoa maelezo polisi ila leo ndio siku ya kutoa ushahidi mahakamani.
Hakikisha pia uwe umeshawaaga wana Familia wako ( hasa nani wa kukuletea Ugali, Maharage, Dagaa na Tembele ukiwa Rumande au Gerezani ) kwani kwa Ushahidi ambao unaenda Kuutoa huko Mahakamani na hivi unavyoonekana Unaogopa na huna a, b, c's za Kesi na Ujibuji wa Maswali unaweza ukajumuishwa na huyo unayeenda Kumtetea na tusikuone tena Ukichangia hapa JamiiForums.
 
Wanasheria wa Serikali hutengeneza maswali na majibu kisha humpa shahidi akajibu kadri ya walivyo muuliza. Lengo la Wakili wa Serikali ni kushinda kesi kwa manufaa ya Serikali.

Kamwe usijibu kadri ya alivyokuandaa bali jibu kadri ya ukweli unaoujua. Ukifanya sivyo utakutana na cross examination ya upande wa pili, itakuumbua tu na utaonekana huna thamani.

Pili usitumie akili zako sana kukumbuka kitu, kama umesahau unasema sikumbuki. Maswali mengi ni ndiyo na hapana
 
Hakikisha pia uwe umeshawaaga wana Familia wako ( hasa nani wa kukuletea Ugali, Maharage, Dagaa na Tembele ukiwa Rumande au Gerezani ) kwani kwa Ushahidi ambao unaenda Kuutoa huko Mahakamani na hivi unavyoonekana Unaogopa na huna a, b, c's za Kesi na Ujibuji wa Maswali unaweza ukajumuishwa na huyo unayeenda Kumtetea na tusikuone tena Ukichangia hapa JamiiForums.
ingekuwa hivyo watu wasingeenda kutoa ushahidi
 
Kufa sio tatizo, nikifa leo yeye atakufa kesho tutatofautiana siku ya maziko tu,
Sikihofii kifo kwa sababu najua kipo na lazima kinikute.

Nb
Sio kesi ya viwanja ni kesi ya vijana wa hovyo wasioweza kufunga zipu zao vizuri ata kwa watoto wadogo.
Pia usisahau kuwaambia kuwa yote haya ni matokeo ya Uzi wako wa kula kimasihara ndio umetengeneza vijana wengi wa hovyo nao wanataka kujaribu mwisho wanafanya ivyo.
 
Mahakamani hawasalimiiii..usije salimia mtu ukienda kule.

Toa ushahidi ulio uona kwa macho,kesi nzito hiyo utaulizwa maswali na mawakili (kama wapo) au na mshtakiwa utaku uliza.. mjibu na akikukatalia usimwambie kwa jazba wewe ni muongooooo.. Mkamate kwa maswali

Sheria haina huruma, wala haipokei viapo we ukimwambia hakimu HAKI YA MUNGUUU MUHESHIMIWA NIMEMUONA hakimu hatambui.hilo anataka umueleweshe kwa kumdaka mshtakiwa.

Najua unatamani mshtakiwa aingie Kingi, usijipange sana kuhusu Wewe, Andaa maswali ya kumtandika mshtakiwa ili hakimu ajue kweli katenda kosa

Wewe utasema ulichooona kisha hakimu atamuuliza mshtakiwa una la kumuuliza? lazima aseme ndio, Atakuuliza maswali ambayo najua utayajibu yote (kama wewe sio shahidi wa mchongo)

Akimaliza Hakimu akuruhusu na wewe umuulize maswali Asipo kuruhusu nyoosha mkono mwambie muheshimiwa naomba kumuuliza mshtakiwa maswali kabla sijatoka mbele ya mahakama yako...

Mtandike maswali ambayo live live yatamtia kingi. Shahidi usikae kimya shindilia maswali kwa mshtakiwa ndio utaweza Mfunga ukienda tu ukasimama wima kama HAKIMU kashakula HELA ya mshtakiwa UJUE hizo ndio weakness point anazotumia HAKIMU kumuachia mshtakiwa.

Shahidi ndio unaweza mfunga mshtakiwa kwahyo pangilia maswali yako ya kibabe ya kwenda kumshindilia mtu, wewe hauna ishu zaidi ya kufika kusimama kuelezea ulichoona na kuanza maswali na majibu baina yako na mshtakiwa.
 
Wanasheria na wazoefu ambao mmewahi fika mahakamani, nimepigiwa simu na mwanasheria wa Serikali niende nikatoe ushahidi.

Kuna tukio lilitokea na mimi ni mmoja kati ya walioshuhudia.

Kipi cha kuzingatia wakati wa kutoa ushahidi.

NB: Nilishatoa maelezo polisi ila leo ndio siku ya kutoa ushahidi mahakamani.
Kuwa, na, kitambulisho chako chochote, pili SEMA ukweli tu, usitie chumvi wala kuongea uongo.
Wakati wa cross examination(kuhojiwa, na, wakili wa utetezi), usipaniki, kuwa kawaida tu.
 
Back
Top Bottom