Nipo njia panda kuhusu kuendelea kuishi ghetto. Ushauri wenu unaitajika

Nipo njia panda kuhusu kuendelea kuishi ghetto. Ushauri wenu unaitajika

nyasangaboy

Senior Member
Joined
Jul 14, 2020
Posts
127
Reaction score
58
Habari zenu wadau, nilikuwa naomba ushauri kutoka kwenu wadau ni hivi ninapoishi kodi yangu inakaribia kuisha nataka kurudi nyumbani kwa mzee. Na sababu ya kutaka kurudi nyumbani na kuacha kupanga kwa sababu ya kutokuwa na kazi kwa sasa so hela ya kodi sina.

Lakini girlfriend wangu amekataa nisirudi nyumbani niendelee kupanga yeye atanisaidia Kodi, so nilikuwa naomba ushauri niendelee kuisha kwa kulinga unga ghetto au nirudi tu nyumbani nikajipange upya.
 
Rudi nyumbani upange mipango upya au kuendelea kukaa hapo na kuendelea kuungaunga.
 
Ukirudi tu home ndio imetoka hiyo,utarudi home mara ngapi? ina maana kila utakapokua unakwama solution ni kurudi home? Pambana na una bahati ya kumpata GF mwenye ushirikiano,ingekua mwingine angesha kukimbia,ila kama alivyoshauri mdau hapo juu,usije kumtupa huyo GF wako.
 
Marufuku kurudisha mpira kwa kipa no matter how your life seems to be miserable... Pambana mkuu tena GF wako ameshakwambia atalipia we kubali tu alipe hiyo kodi usiwaze habari za nitaonekana "marioo"
 
Shukuru Mungu umepata mwanamke anayejitambua. Unarudi nyumbani kufanya nini? Kumbuka hata baba yako na mama yako walipitia changamoto hizi lakini wakakaza na hawakutaka kurudi nyumbani, walikopa na kufanya kazi zozote ili wapate ridhiki kipindi hicho cha hali ngumu na kilipita.
Baki kwenye gheto lako na fanya kazi yoyote ile inayokuja mbele yako. Hakuna pesa inayopatikana kirahisi kwahiyo ni kupambana tu.
 
Hongera sana kwa huyo GF wako kwanza anakupenda sana
Jitahidi ukomae mjini jishulishe kwa lolote kodi ikishalipwa mengine yatapatikana.

once again mpende sana GF wako kwani anakupenda kitendo cha kumwambia unarudi nyumbani kilitosha kukukimbia. Maana unajiuliza changamoto kidogo unataka kurudi nyumbani what if wazazi wako hawapo hapa mjini? Komaa ushakuwa mkubwa
 
Ukirudi tu, umeisha. Endelea kuwa mario tu, manzi akulipie kodi. Ila usije ukamtupa ikiwezekana oa huyo huyo. An future plans na mipango mema na wewe
Sio kwamba naishi Naye hapana nipo mwenyewe na kazi sina kwa sasa so naona mwanzo wa stress
 
Hapo sasa!! ni heri uombe assist kwa kipa kama ipo usaidike lakini sio ukusanye virago urudi muanze kupishana koridoni na kipa. Haipendezi..
Sasa kama mambo hayaeleweki si ndo mwanzo wa stress
 
Usifanye kosa kurudi nyumbani, kama mpenzi wako atakusaidia ni sawa ila pambana mpaka kieleweki usije itwa marioo na huyo binti umuoe kabisa ni wife material sio material wife.
Shukrani kwa ushauri murua mkuu
 
Back
Top Bottom