Usirudi nyumbani, maisha yanaenda mbele hayarudi nyuma.... pambana kama vile wazazi wako hawana pa kukuhifadhi
Kazi ni ngumu siku zote, ukubwa ni majukumu mwanangu. Pambana kadri uwezavyo, umri ungali mdogo fanya hata vibarua visivyo rasmi !!
Girlfriend anaweza kukusaidia lakini iwe umeshindwa kabisaa na isiwe mazoea. Unaweza hata kutafuta chumba cha bei rahisi zaidi ili mradi tuu paitwe nyumbani kwa
nyasangaboy . Wanawake tumeumbwa tofauti kidogo, kuna vitu tunaweza kufanya tukiwa na mapenzi lakini vikija kutuchosha inakua aibu kwa mwanaume-uchebe anaelewa.
...ukiweza pambana sana usimame mwenyewe maana ndio maandalizi ya ubaba hayo. Itakujengea kujiamini na heshma pia. Baba bora ni yule anayeweza kusimamia mipango ya nyumba yake na kumuongoza mke wake kwa matendo
Huyo gf anakupennda tunza sana moyo wake. Usimbadilishe