Nipo njia panda wajasiriamali nisaidieni natamani kurudia tena uwekezaji huu wa kuku ila nasita

Nipo njia panda wajasiriamali nisaidieni natamani kurudia tena uwekezaji huu wa kuku ila nasita

Mzee wa kusawazisha

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
1,601
Reaction score
1,172
Kama uzi unavyojieleza. Salam! Wana jf.. Najua Kuna watu wamenizidi umri humu bas shikamooni

Kwanza kabisa mi ni mwanafunzi wa chuo mwaka wa 3 na wa mwisho, nilipanga mwaka wa 3 nianze kufuga kuku ili wa nisaidie apo mbeleni katika pesa nazopata za kujikimu (boom).

Ni kweli pesa za awam ya kwanza nilinibana Sana Nika tenga laki mbili nikaanzisha mradi wa kuku Kwa bahat Mbaya wale kuku walikufa wote,

Sasa nimepata tena laki mbili zingine wakuu na mda unazidi kusonga Sana Saiv ni January mwezi wa 7 namaliza chuo nikiwaza tena kununua kuku nawaza jinsi awam ya kwanza ilivyokua japo siwez kusema watakufa tena ila wasi wasi ni muhim maana mimi ni mwanadam

Nishaurini je nirudie tena kwenye kuku kule kule au nifuge mfugo gani ambao naweza kupata faida ndani ya miez 7?

Nb. Kuku awam ya kwanza niliwapa dawa, za aina yote ila yakatokea hayo niliyoleza apo juu..

Kiukweli lengo langu mwezi wa wa 8 mwaka Huu Mungu akipenda nipate mtaji ambao utatokana na uwekezaji huo mtakao nishauri kama nilivo Omba apo juu

Asante Sana kwa watakaonisaidia Kwa mawazo Mazuri yenye kunijenga asanteni.!
 
Nilinunua sehem ambayo sio nzuri mkuu m1 alikua mgonjwa akaja kuambukiza wote
Hapo tayari umegundua chanzo unacho paswa kufanya ni kununua wote kwa wakati mmoja au sehemu moja ili hata kinga na tiba uwape kwa pamoja

Hii itakusaidia wewe kuratibu kinga kwa wakati mmoja
 
Nilinunua sehem ambayo sio nzuri mkuu m1 alikua mgonjwa akaja kuambukiza wote
Sawa mkuu, sasa kuwa makini na kuku ambao utawanunua term hii wasije wakafa kama walee.... ugonjwa wa kideri sio ugonjwa mzur ni sawa na kipindu pindu.....

Pia usiyahofu yajana maana hata yaleo yanaogofya sana kwa watu wengine....
 
Mkuu awo niliwanunua sehem 1 Kwa pa1
Sawa inawezekana ulichelewesha kuwapa kinga maana hii hutokea sana ukichelewa kuwapa kinga

Na wakati mwingine unapaswa uhakikishe kinga na tiba unazitengeneza mwenyewe na kuwapa ukiagiza mtu anaweza akalipua na dawa isifanye kazi na ukapa hasara
 
Mkuu mimi Ile Ile nawanunua na kuwaanzishia Kinga... Na ninichosita zaidi ni lile banda nahisi Kuna mabaki ya vijidudu
 
Walikuwa kuku wa ngapi?

Wa umri gani?

Baada ya mmoja kufa ulimpeleka kwa Dr kujua ni ugonjwa gani unawaua?

Kabla ya kuanza kufuga ulipata ushauri wowote kwa mtaalamu/mfugaji?
 
Walikuwa kuku wa ngapi?

Wa umri gani?

Baada ya mmoja kufa ulimpeleka kwa Dr kujua ni ugonjwa gani unawaua?

Kabla ya kuanza kufuga ulipata ushauri wowote kwa mtaalamu/mfugaji?
Walikua kumi mkuu na matetea wanaokaribia kutaga.. Sikupeleka Kwa doctor ila kilikua kideri mkuu niliwapa dawa ila haikusaidia kitu
 
Nilinunua sehem ambayo sio nzuri mkuu m1 alikua mgonjwa akaja kuambukiza wote
Hii kitu iliwahi kunigharimu,nilipoteza nusu ya kuku kwenye banda langu,lakini bado ilikuwa nisomo kwangu kwani sasa hivi nafanya vizuri kiasi..
 
Back
Top Bottom