Hata hatujuwi dhamana yake ilikuwa kiasi gani? 700, 800 au 900?! Au Buku mia nane?...What a guy...Kwenye maisha yangu sijawahi kupigiwa vigelegele, kupepewa na leso, kuonyeshwa kwenye luninga wala kuzungumziwa katika kila kona TZ, mpaka waTZ wa ng'ambo wanamzungumzia huyu bwana, kwenye twitter yupo, instagram yupo, facebook yupo, snapchat yupo, radioni yupo, luninga yupo, serikalini anaongelewa, polisi wakimtazama wanacheka wenyewe, YONO ndio wamemkimbia kabisa, hata hawana hamu naye, wako kimya. Kwa kweli nampa pongezi, hata siku akiitwa na Mwenyezi Mungu ashatengeneza historia, cheers Dr. Shika...