Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Kuna siku nilienda mkoa flani sasa ile ndugu wanakufosi unafikiaje Lodge na sisi tupo? nikaona sio kesi acha nifikie kwao nikawa natoka usbh narudi usiku siku ya kwanza wakaleta chapati mbili mbili na maharage na chai nikasema poa sio mbaya labda uzungu kesho tena ivo ivo na siku ya tatu vile vile nikaaaga inabidi kesho twende wilayani sina uhakika kama tutarudi au tutalala huko huko, asbh nikatoka na begi langu nikahamia Lodge mbali kidogo na wanapoishi nimekaa siku tatu sasa siku moja jioni nazungukia bar za pale mjini nikakutana na baba mwenye nyumba akashtuka upo ikabidi nizuge ndio tumeingia muda huu tunatafuta chakula tuendelee na safari.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Mkuu hao walikuwa wapare wenzakeo hao. Jamani kula Kwa mpare ni KAZI aseee chakula Chao kidogo oooo wanabana matumizi wale Watu tena ukute mpare msabato aseee utajuta. Kande halijaungwa na kisamvu hakijaungwa
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] haaaaaaah haaaaaah dah nimecheka kama fala

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Mac Alpho sijui kwanini tu nimekumiss hapa baada ya kuona hii thread... 😂😂
Nimeona heading tu nikajiikuta nacheka sana, ngoja nikaisome sasa😄.

UPDATE:

Sijui ni aina ya watu na familia? By nature tu kila sehemu(miongoni mwa familia) ni walaji haswa, kwahiyo sijawahi kukutana na hii kasumba ya mleta mada.

Binafsi najua kabisa kuwa, hata mimi na wewe tusingetoboa kwenye huo mji😄.

MAISHA NI MAGUMU, mleta mada aelewe hilo.
 
Wenzako wanarudi wameshiba na hata wakikaribishwa mezani wanapiga tonge mbili tuu kuweka heshima tuu usionekane una dharau, haya mambo ya chakula, remote ya TV au kutumia bafu wakati kila mtu anajitayarisha kwenda kazini lazima uwe makini sana, muhimu soma mazingira haraka haraka
 
Nimeona heading tu nikajiikuta nacheka sana, ngoja nikaisome sasa😄.

UPDATE:

Sijui ni aina ya watu na familia? By nature tu kila sehemu(miongoni mwa familia) ni walaji haswa, kwahiyo sijawahi kukutana na hii kasumba ya mleta mada.

Binafsi najua kabisa kuwa, hata mimi na wewe tusingetoboa kwenye huo mji😄.

MAISHA NI MAGUMU, mleta mada aelewe hilo.
😂😂😂😂😂😂
Nasikitika kusema Mimi ningetoboa, si unanifahamu vyema lakini vile ambavyo mie siyo mlaji kabisa...??

Ahsante..!!
 
Kwani lazima ule ww ushawaletea zawadi na umeona msosi mdogo ikifika mida ya jioni tafuta sehemu kula kitimoto yako kilo na ndizi mbili ukisindikiza na coke ya baridiiiii mchana tafuta hata mama lishe kula wali wako hapo nyumbani wana bajeti zao temana nao kabisa.

Mimi nilikua nikienda kwa shangazi yangu asubuhi natoka nachukua mikate miwili mmoja wa kwao mmoja wangu nanunua na blueband au peanut butter nikifika muda wa chai naiweka yote mezani wanaanza kuleta bajeti eti mmoja ubaki hapo ndipo nawaambia huu nakula mwenyewe ili nisiharibu ratiba zenu huo kuleni nyie mwanzo walipata tabu ila walizoea mchana natoka nikirudi jioni napitia sehemu ya nyama au kuku naagiza chakula najipigia nikirud home nimeshiba nagusa gusa vijiko viwili nalala nikiwa njema kabisa. Kama huna hela kufa njaa tu hamna namna
Sasa gharama yote hiyo ya nini, si ukae lodge tu.
 
Back
Top Bottom