soma maabdiko haya:
Waefeso 6:10-12 yasema, "hatimaye, mzidi kuwa hodari katika bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."
marko 16: 15- 18 "nendeni ulimwenguni kote mkahubiri habari njema kwa kila mtu. Anayeamini na kubatizwa ataokolewa; asiyeamini atahukumiwa. na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini: Kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya. Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona."
sali sala ya kufukuza jini mahaba kila unapolala:
" bwana yesu nipo mbele yako< ninatubu dhambi zangu zote, unisamehe, naomba uniponye katika kila aina ya ungonjwa "(taja kile kinachokusumbua)...asante kwa kunisamehe ...naileta kwako nyumba yangu, familia yangu, ukoo wangu uniokoe...naleta kwako mwili wangu uniponye, unisaidie katika masomo, kazi, biashara zangu nk....naomba unibariki kama ulivyobariki maji yakawa divai katika ile harusi ya kana ya galilaya,..naomba unipokee, unipe matumaini mapya nikafurahie maisha kwa kadri ya mapenzi yako, nafunga nguvu zote za shetani juu yangu asipate tenafasi ya kunitawala mwili na roho yangu..nakemea nguvu za mapepo, nakemea nguvu zote za giza..zikashindwe juu yangu ..najitoa kwako ehee bwana yesu..nipiganie...unirehemu, napokea haya kwa moyo wangu, katika jina la baba, mwana na roho mtakatifu...amen!!.
Jione upo huru sasa na umepona kila ugonjwa kwa jina lake yesu wa nazareti aliye hai.
Amen