Nisaidieni kujua kwanini huyu kaka kaniganda kwa miaka minne

Qashy Lilith

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2024
Posts
1,508
Reaction score
2,965
Habari zenu Wana Jf naomba nieleze kwa ufupi ...Mimi ni binti WA kike ila Kuna mkaka nilikiwa nae kwenye mahusiano nikiwa sekondari ila nlimuacha baada ya kugundua alinificha kuwa alikuwa na mtoto

Mara kadhaaa tangu kuachana nae amekuwa akinitafuta kwa miaka minne tokea 2020 na kusem kuwa anatka kunioa ila kila akinitafuta namwambia sipo Tyr kwa ndoa ...nikmwambia sitaki ndoa anakubali kabisa hatnisumbua tena ila baada ya siku kadhaa bado anarudi na lile lile swala lake la kunioa ..
Je huyu mkaka atakuwa amemaanisha kunioa au anataka kuniigiza Cha kiume?!
 
Aise hivi kumbe kuna wanaume bado wana lilia ndoa! Ama kweli dunia haishi vituko.
Huyo mkubalie haraka sana kabla jua halijazama kupunguza idadi ya single maza baadae.
 
Olewa shauri yako usine ukawa gazeti la jioni miaka inasonga na value yako inashuka
 
Kakupenda.

Kwani kuna wanawake wangapi mtaani wenye kiu ya kweli kwa mahusiano ya ndoa, hajawaona, kwanini wewe tu, haujiulizi?

Wee endelea na msimamo wako huo usio na mashiko, akichoka kukufuatilia, upendo wake kwako utadrop na kufanya maamuzi mengine.
 

Subiri ukichinda utakuwa na majibu; ukithibitisha mwanaume anakupenda usimkatae, ila usikubali kufunuliwa kirahisi, wakati mwingine Speed zote hizo ni akufunue tu akute arufu aende!
 
Acha nimshikilie basi🙂‍↔️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…