Nisaidieni mawazo yenu

Nisaidieni mawazo yenu

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30 nimeajiriwa.

Baba yangu amegoma kabisa kujenga nyumba yake akidai mimi nisipomjengea watu watanidharau na kunicheka, yaani kwa ufupi nawaza mpaka nakonda ukizingatia kwa sasa namjengea mama ambaye tayari walishaachana na baba.

Mama naye alikuwa anaishi mazingira magumu kupita kiasi ikabidi nimsitiri japo nyumba yenyewe bado haijaisha vizuri.

Sasa baba anaishi mazingira magumu sana (nyumba mbovu) kipato changu ni kidogo sana na mimi binafsi sijajenga, nashindwa kupata majibu wakuu nikisema nianzishe tena nyumba ya baba na ya mama ambayo bado haijaisha, nitashindwa kuwaandalia watoto wangu mahali pa kukaa.

Nishaurini ndugu zangu.
Kama baba yako alikusomesha akakutunza akakuleaa akatumia rasimali zote ili usome akajinyima akakuwezesha kufika hapo huna budi kumjengea kwani bila yeye wewe usingefika hapo.........

Lakini sasa kama hakuwa na msaada na wewe basi we muache na maisha yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo nyumba unayoijenga ungeiita nyumbani bila kuigawa kwamba ni ya mama au baba. Ikishakamilika unawaambia hapo ndio umeshatengeneza makazi umenawa anaetaka aishi hapo. Si kila mmoja na chumba chake?

Baada ya hapo anza kufanya mambo yako.
Mzazi atakaegoma kuishi hapo hatakulaumu, wewe utabaki pale pale kwamba nyumba umeshawajengea.

Huwezi kuwafurahisha watu wote wakati wote, uwezo na rasirimali za kufanya hivyo hazipo. Hapo ndio umuhimu wa vipaumbele unapokuja.

Utajikuta unashindwa kusomesha wanao na wewe mwenyewe msongo wa mawazo ukakusababishia maradhi sugu ukaja kuanza kulaumu wanao siku za usoni.

Lakini hizi familia zetu za kiafrika shida sana, ndio maana minyororo ya umasikini haituachii vizazi na vizazi.
 
Kwenu mmezaliwa wangapi????
Kama una ndugu zako shikiriana nao kumjengea mzee.
Ila pia Jenga kwako kisha mchukue baba uishi nae. Yani kuachana kwao kukuumize wewe kujenga nyumba mbili?
Nyumba ya mama ina jina la nani? Kama ina jina lako ungewaomba waishi pamoja....naamini wanakuchukulia kama mtu mzima kuna namna ukiongea nao wataheshimu na kukusikiliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana jitahidi kadri uwezavyo usifanye mambo ambayo yako nje ya uwezo wako.
 
Wazazi wameshatengana, well... mama anaishi na nani na mama anaishi na nani..?

Ukinijibu vema nitarudi.
 
Roho mbaya sio poa
Sio roho mbaya,

Jipe muda wa kujipanga na kupambana.

Siku mambo yakishakua mazuri,

Unakua msaada sana Kwao kiroho Safi bila manung'uniko.

Sasa hio misaada yenyewe mnayojifanya mnatoa huku uwezo wenyewe hamna,

Afu mkitoka hapo mnanung'unika, Kiukweli hata kwa Mungu Haina Thawabu.

KAMA KIJANA,
WAPOTEZEE NDUGU KWA MUDA HUKU UKIPAMBANA KWA JASHO NA DAMU

MAMBO YAKISHAKAA SAWA, WAO WENYEWE WATAFURAHI TU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm mshua alizima, baada ya 40 kwenye kikao cha familia, Mama Mlezi alinipa nafasi nitoe maoni yng kuhusu mgao wa Mali.

Kumbuka huyu Mama si Mamangu Mzazi, ila amezaa na Mzee watoto wawili! Kulikuwa na Nyumba 2, pick up, mifugo, mashamba na power Tillers!

Mi nliwaambia vyote vilivyopo vitumike hapa hapa Kijijini kumtunza Mama na waliopo, hakuna haja ya mgao! Mpk leo wananipenda ile mby!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazazi wameshatengana, well... mama anaishi na nani na mama anaishi na nani..?

Ukinijibu vema nitarudi.
Baada ya kuachana baba anaishi mwenyewe hajaoa tena na mama pia anaishi peke yake hajaolewa tena
 
Mm mshua alizima, baada ya 40 kwenye kikao cha familia, Mama Mlezi alinipa nafasi nitoe maoni yng kuhusu mgao wa Mali.

Kumbuka huyu Mama si Mamangu Mzazi, ila amezaa na Mzee watoto wawili! Kulikuwa na Nyumba 2, pick up, mifugo, mashamba na power Tillers!

Mi nliwaambia vyote vilivyopo vitumike hapa hapa Kijijini kumtunza Mama na waliopo, hakuna haja ya mgao! Mpk leo wananipenda ile mby!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo huna unacho miliki mzee kaka!??
 
Upo peke yako katika uzao wa mama na baba yako?

If yes,

Jitahidi hata kuiboresha hio iliyopo na umweleze mzee plan za kumjengea as time goes.

FYI,

Usipokuwa makini, mzee ànaweza kufa (siombei) akakuachia laana (inawatokea wengi, kutokana na manung'uniko ya wazazi) ambayo itakuvurugia maisha!

Jipange mapema

Duh! Sawa ntajitahidi sana kuepuka laana japo baba ashaongea mengi juu yangu anahisi nambagua ila nkirudi Tanga likizo ntajilipua vyovyote sina jinsi hali mbaya za wazazi zinanyima raha sana
 
Sio roho mbaya,

Jipe muda wa kujipanga na kupambana.

Siku mambo yakishakua mazuri,

Unakua msaada sana Kwao kiroho Safi bila manung'uniko.

Sasa hio misaada yenyewe mnayojifanya mnatoa huku uwezo wenyewe hamna,

Afu mkitoka hapo mnanung'unika, Kiukweli hata kwa Mungu Haina Thawabu.

KAMA KIJANA,
WAPOTEZEE NDUGU KWA MUDA HUKU UKIPAMBANA KWA JASHO NA DAMU

MAMBO YAKISHAKAA SAWA, WAO WENYEWE WATAFURAHI TU.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa dwag
 
Back
Top Bottom