Nisaidieni mawazo yenu

Nisaidieni mawazo yenu

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30 nimeajiriwa.

Baba yangu amegoma kabisa kujenga nyumba yake akidai mimi nisipomjengea watu watanidharau na kunicheka, yaani kwa ufupi nawaza mpaka nakonda ukizingatia kwa sasa namjengea mama ambaye tayari walishaachana na baba.

Mama naye alikuwa anaishi mazingira magumu kupita kiasi ikabidi nimsitiri japo nyumba yenyewe bado haijaisha vizuri.

Sasa baba anaishi mazingira magumu sana (nyumba mbovu) kipato changu ni kidogo sana na mimi binafsi sijajenga, nashindwa kupata majibu wakuu nikisema nianzishe tena nyumba ya baba na ya mama ambayo bado haijaisha, nitashindwa kuwaandalia watoto wangu mahali pa kukaa.

Nishaurini ndugu zangu.
Yeye alimjengea baba yake?
Pole..Kuna wazazi wanajua kukwaza watoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani aliyekusomesha. Baba yako anajishighilisha na Kazi gani na mama yako anafanya Kazi gani
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30 nimeajiriwa.

Baba yangu amegoma kabisa kujenga nyumba yake akidai mimi nisipomjengea watu watanidharau na kunicheka, yaani kwa ufupi nawaza mpaka nakonda ukizingatia kwa sasa namjengea mama ambaye tayari walishaachana na baba.

Mama naye alikuwa anaishi mazingira magumu kupita kiasi ikabidi nimsitiri japo nyumba yenyewe bado haijaisha vizuri.

Sasa baba anaishi mazingira magumu sana (nyumba mbovu) kipato changu ni kidogo sana na mimi binafsi sijajenga, nashindwa kupata majibu wakuu nikisema nianzishe tena nyumba ya baba na ya mama ambayo bado haijaisha, nitashindwa kuwaandalia watoto wangu mahali pa kukaa.

Nishaurini ndugu zangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mjomba ukitaka kufanya kwa pamoja utashindwa sasa cha kufanya ww ndo uwe daraja la kawaweka pamoja na uaambie ukweli wote ni wazaz wangu lakn kufnya jambo ambalo liko nje ya uwezo wangu ntashindwa na pia naomba mkaa pamoja hapa kama kijana wenu mungu kanibariki na haiki kidogo naomba tukitumie wote kwa pamoja .
 
Back
Top Bottom