Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Hii nyumba ninayoishi tupo wapangaji watatu kwenye compound moja. Nimehamia hapo huu ni mwezi wa pili unaenda kuisha.
Ndani ya hizi wiki chache, nimeona mabadiliko makubwa ya matumizi ya umeme. Mwanzoni ilikuwa natumia wastani wa unit 2.4 kwa siku, ila kwa sasa imepanda mpaka 3.6 kwa siku.
Nimeona sio kawaida, mpaka nimehisi kwamba inawezekana kuna jirani ananipiga umeme wangu, na ushahidi nilionao ni kwamba, mahali ilipo mita yangu ipo pamoja na jirani yangu mmoja, ila sasa maajabu nashangaa hii siku ya pili nimechunguza, hiyo mita ni kama unit za umeme za jana ndo zipo leo. Nikimaanisha kwamba, ni kama vile huyu jirani atakuwa anatumie umeme kwenye source ingine ambayo possibly ameconnect umeme wangu.
Nnachokifikiria kwa haraka haraka ni kumleta fundi wiring ili akague system nzima ya umeme wangu.
Naombeni mnipe mbinu zaidi wakuu, nimekereka sana kuligundua hili, kitendo cha mtu kuniibia huwa nakichukulia kama kuniona sina akili na kunitusi.
Nahisi kama nimuadabishe bila kumuambia chochote. Haiwezekani mtu ufikiria kupambana na maisha halafu ufikirie tena kupambana na majirani wezi.
Mbinu safi na chafu nazipokea ahsante