Nisaidieni mbinu za kupambana na huyu jirani 'mwizi wa umeme'

Kama ni usiku na amewasha taa na unahisi atakua anatumia umeme wako, nenda kwenye main switch zima kisha cheki kama jirani kuna giza
 
Kama wiring ya nyumba ni ile inakua shared na wall sockets za chumba zaidi ya kimoja basi inawezekana kachomeka extension na friji lake, tv na subwoofer la Sea Piano vyote vinafadhiliwa na wewe.

Yaani yeye units zake zinasoma kwenye taa tu.
 
Nafatilia nasubiria mrejesho. Mtu kuiba umeme waziwazi hizo Ni dharau Kama ni kweli
 
Kwahiyo jirani ndo umekuja kunitisha na huku ili nisikudhibiti?

Sasa kwa taarifa yako, lazima nilete fundi akague. Kama ulikuwa huna bajeti ya umeme anza mapema kuitafuta.

Naenda kukata mirija ya umeme wa kitonga
Huna lolote mkuu.. huo umeme unaotumia ni wakwako kabisa we lipa bili. Kwanza unamavitu mengi ya umeme unashangaa nini bili kua kubwa? Jikaze kiume 🤣🤣
 
Anayekuibia umeme siyo lazima readings za mita yake zibaki constant.
Inawezekana huyo mwizi mita yake akaibebesha mzigo wa vifaa visivyokula umeme. Hivyo mita yake itasoma units kidogo na mita ya Mushi akaipiga mzigo kisawa sawa na ikasoma units nyingi.
 
NJIA sahihi ni kukagua system.

Inawezekana huyu jirani yake ka connect waya wa kwenda kutumia device moja au mbili wenda jiko au friji huku system nyingine iki fanya kazi sawa..

Kama kafanya hivi basi jamaa kwa kutumia mbinu ya kuzima, au kusubiri uneme uishe bado hato pata jawabu ikiwa jamaa ame connect na friji au jiko la kupikia.
 
Hapo sawa sawa..sasa nishauri hapo.. itakuwa wizi umefanyika kwenye waya huo mkubwa?
 
Kama wiring ya nyumba ni ile inakua shared na wall sockets za chumba zaidi ya kimoja basi inawezekana kachomeka extension na friji lake, tv na subwoofer la Sea Piano vyote vinafadhiliwa na wewe.

Yaani yeye units zake zinasoma kwenye taa tu.
Hii ndo nahisi imefanyika, yaani wizi umefanyika kwenye socket ambazo tunashare kuta.. nataka nilete fundi ikibidi nikate nyaya zote za socket ambazo zinaenda upande wa nyumba yake ilipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…