Nisaidieni mbinu za kupambana na huyu jirani 'mwizi wa umeme'

Au inawezekana huyo mshkaji wako ana hela ya kutosha kutop up umeme kila siku...
hali ngumu za kimaisha zinaweza kukufanya uone watu wote wanaoijiweza ni wezi..............
 
So solution hapa ni kuleta fundi akague.. haswa haswa zile nyaya ambazo zipo karibu na nyumba ya mshikaji..
 
Au inawezekana huyo mshkaji wako ana hela ya kutosha kutop up umeme kila siku...
hali ngumu za kimaisha zinaweza kukufanya uone watu wote wanaoijiweza ni wezi..............
Hamna haipo hivo.. nimetafiti mkuu.. nna uhakika na hili swala kwa asilimia zaidi ya 70.
 
uko sahihi chief!
 
Baada ya kutoka kwenye Luku, umeme ni wako, fuatilia huenda kuna mahali kachubua waya ambao ni"life" na kukuibia.
 
Hamna aisee huyu sijui atakuwa kabila gani.. halafu ni jamaa fulani yaani ukimuona huwezi kudhani anaweza kuwa anaiba umeme.
Kuwa nae makini mkuu,ukimbaini afunguliwe kesi ya uhujumu,mkuu kama umeoa kuwa makini na Huyo jamaa aisee.
 
Usimuhisi mwenzio kuwa mwizi.

Jihakikishie. Cha msingi muite jilani yako mujadili mambo mengine mengi kuhusu upangaji na changamoto za Umeme.

Maswala ua kuuliza kuhusu umeme ili usiharibu ujilani ni kama ifuatavyo.
1. Aisee tangu nihamie hapa umeme unaenda sana, vipi na wewe ni hivyo ama ni kwangu tu?
2. Nataka nilete fundi akague wiring, nijue kama imechoka ama la.
3. Mwambie akuleleze uzoefu wake kuhusu umeme wa hizo nyumba.

Hapo utapata reaction yake na kuelewa nini kilichopo Nyuma ya pazia. Vilevile utaona umeme wako unaenda vizuri maana kunauwezeekano akaacha kutumia umeme wako,
 
hahahahhaaa...mchagga akiibiwa anahaha balaaa.......usiwe na papara....unit kwako inaweza soma zero but kwake hauzimi...why?? sbb huo mchepuko wa wire unaweza kuwa unakwenda kwenye item 1 au 2!! yes, fridge au jiko....so hiyo kwake ni internal....atajua mwenyewe kimya kimya....ukinunua kwake kama kawa......ita fundi akague bila wewe kumwambia unahisi kuna uhalifu unaendelea....yeye agundue kwanza (fundi)....ukigundua pigisha shoti vitu zake then kimyaaaaa....hiyo diversion unaiacha unakata kwenye mainswitch....upanga kwa upanga....
 
Mkuu mimi na mbinu chafu tu za kukabiliana na huyo mwizi umeme (Kishoka).
 
Mkuu...Hilo tukio huenda likafanana na tukio hili, kuna mpangaji mmoja alipanga kwenye nyumba sehemu ya ukumbi mkubwa,ambapo anatumia kuonesha move na mpira,Sasa ukumbi anaotumia na nhyumba niliyokuwa nimepanga wanatumia luku moja......alichokifanya alimwita fundi akafanya makarateee yakeee.......na kisha akaweka luku yake......mziki ukawa hapaaa sasaaa, tukiweka umeme,tunatumia wote. Ukiiisha umeme wetu,anaponyeza sehemu,anatumia WA kwakwe. Tukaja kustuka baada ya kuona mbona umeme ukikatika kwetu,kwa maana ukiiisha na yeye unakata kwakwe,lakini baada ya dk 2, kwakwe yanarudi na kuendelea na kaziiii.....tulimwashia motooo,wakaja tanesco wakamkamata hiyo jamaa....akapigwa fainiiiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…