Kila kitu kilikuwa kama maigizo kabla ya kuona rasmi napokea muamala kama mnavyoona hapo juu. Sina la kusema zaidi ya kuwashukuru JamiiForums kwa kunipatia hela hii ambayo sitahitaji ushauri wa jinsi ya kuitumia.
Nimefungua akaunti hii muda mrefu sana, nikawa napata vijisent vya hapa na pale kwa kuandika tafiti nikiwa na wenzangu ambao kwa sasa kila mtu ameajiriwa kimpango wake.
Nashukuru kwamba sijaacha suala la kuandika na kupitia Stories of Change nimepata hiki kiinua mgongo ambacho kinatosha kuanzisha walau kampuni tuliyowaza kuianzisha.
Naomba niwaambie kuwa mimi ni mtafiti, nimeshapublish zaidi ya paper moja kwenye reputable journal, pia nimepresent majukwaa mengi ya kimataifa. Kwa mwaka huu nimefanya presentation mbili.
Naomba ieleweke kuwa bado naendelea kushauri wanafunzi wa post graduate kuhusu tafiti, aidha kama taasisi inahitaji kupata tafiti na pia nasaidia kufanya statistical analysis kwa software yoyote unayoihitaji. Ukitaka training ya matumizi ya software tafadhali nicheki Instagram au kwa namba yangu ya simu ambayo ipo kwenye posts zilizotangulia humu.
Karibuni inbox au kokote kwa kupiga story, kubadilishana mawazo na kupeana michongo.
NB: Hela zina matumizi usije kukopa
Nitumie nafasi hii kuwashukuru sana JamiiForums. Kongole kwenu