Hahahaa!
Kusema ukweli haya mambo [hizi mada] huwa yana msimu wake.
Leo jamaa kaliamsha dude dhidi ya wachuchu. Majuzi hapa DaJane naye alilianzisha dhidi ya ‘wanaume wa JF’.
Kuna kipindi pia wanaume waliandamwa sana hadi kupewa majina ya ‘Pugi’, mara sijui ‘Bwana Pepsi’, mara sijui nini...n.k.
Ukiwa objective observer utagundua kuwa jinsia zote huwa zinashambuliana shambuliana.
Hivyo, kimsingi hii mada haina jipya. Haya mambo yameshajadiliwa sana huko nyuma, yanaendelea kujadiliwa, na yataendelea kujadiliwa.
Labda kilicho kipya hapa ni mwanzisha mada tu kuwa tofauti. Lakini maudhui ni yale yale.
Na naweza kuweka dau [licha ya umaskini wangu huu] kuwa huu si mwisho wa mada zenye haya maudhui.
Muda si mrefu atakuja mtu mwenye ID ya mdada na ataanzisha mada ya kuwaponda ‘wanaume wa JF’.
Watch this space.....