Nishauri chochote niache kuyaogopa maisha

Nishauri chochote niache kuyaogopa maisha

Utakuwa sawa tu Ni mapito,baada ya Hapo utabaki unashangaa ulipitaje Hapo, Cha muhimu jifunze Kuomba. kuwa karibu na Mungu wako anatenda makubwa kuliko ujuavyo,utabaki kuwa ushuhuda.
 
amen, nilikukumbuka jana sana na namshukuru Mungu unaendelea vyema. Mungu aendelee kukuponya kabisa ili amani yako irudi kama mwanzo.
Asante, barikiwa sana aisee
 
Wasalaam,

Sijui niiwekaje hii, lakini naogopa tu nikiwaza haya maisha yanatakiwa yaende aje,, na kwanini inakua hivi🤔🤔

Au ni kwasababu nimeumwa sana nimeanza kupoteza matumaini? Ata sijui nawaza nini🙌🙌.

Yaani iko hivi, ni mwezi wa pili sasa unaelekea watatu siwezi kufanya chochote, kazi zangu na shughuli zangu ambazo nilikua nafanya mwenyewe ni watu ndio wananisaidia kufanya (Hakuna hata kimoja kilichopo kwenye mstari,. Kila kitu kimevurugika, Hawafanyi kama ambavyo mwenyewe hua nafanya🥹🥹).

Watu hata nyumbani naona wanalichukulia hili suala kawaida lakini mimi linaniogopesha sana,. Imagine nilikua nasikia vizuri tu lakini saizi sisikii. Eti macho nayo yameanza kusumbua yaani navaa miwani hatakama sisomi kitu🤔 Kwa mfano ndio ikawa hivi hivi mwisho wa siku si na miguu nayo itaanza kutokutembea na mikono kutokufanya kazi (Na vipi kama ikiwa kweli?) Ina maana ndoto zangu zote ndio zitakua zimeishia hapa au?

Niambie au nishauri chochote ili niondokane na hii sijui ndio fear of unknown au nini?

Mhubiri 9:11​

Tena, nimeona kitu kimoja hapa duniani, kwamba wenye mbio hawafaulu katika riadha, wala wenye nguvu hawashindi vita; wenye busara hawapati chakula, wenye akili hawatajiriki, wala wenye ujuzi hawapandi vyeo; lakini wakati wa bahati huwapata wote pamoja.
 
Back
Top Bottom