Nishauri chochote niache kuyaogopa maisha

Nishauri chochote niache kuyaogopa maisha

I think you should take your time off Internet, concentrate kwenye afya yako...
Nikiachana na kushika simu means nitakua nalala tu mda wote from morning to night which is tiresome 😌
 
Pole kipenzi, majaribu kwa binadamu ni ya kawaida. Ila usikate tamaa wala kujiwazia, mambo mabaya ya mbeleni. Kwa Imani yako omba Mungu, kila kitu kitaenda kuwa sawa. Mungu ni mwema wakati wote.
 
Una shida gani specific?
Yaani ni ugonjwa gani unaofanya hadi macho yaache kuona masikio yazibe
Fafanua labda unaweza kupata msaada...instead of generating fear
Wanasema ni Tinnitus kipenzi
 
Pole sana mkuu kwa magumu unayopitia naamini Ni mapito tu baada Muda fulani kila kitu kitakuwa sawa.

Mungu akufanyie wepesi jamani.
 
Wasalaaaam
Sijui niiwekaje hii,. Lakini naogopa tu nikiwaza haya maisha yanatakiwa yaende aje,, na kwanini inakua hivi🤔🤔

Au ni kwasababu nimeumwa sana nimeanza kupoteza matumaini?? Ata sijui nawaza nini🙌🙌,.
Yaani iko hivi, ni mwezi wa pili sasa unaelekea watatu siwezi kufanya chochote,,. kazi zangu na shughuli zangu ambazo nilikua nafanya mwenyewe ni watu ndio wananisaidia kufanya ( Hakuna hata kimoja kilichopo kwenye mstari,. Kila kitu kimevurugika, Hawafanyi kama ambavyo mwenyewe hua nafanya🥹🥹)..

Watu hata nyumbani naona wanalichukulia hili suala kawaida lakini mimi linaniogopesha sana,. Imagine nilikua nasikia vizuri tu lakini saizi sisikii,. Eti macho nayo yameanza kusumbua yaani navaa miwani hatakama sisomi kitu🤔🤔,. Kwamfano ndio ikawa hivi hivi mwisho wa siku si na miguu nayo itaanza kutokutembea na mikono kutokufanya kazi ( Na vipi kama ikiwa kweli???) Ina maana ndoto zangu zote ndio zitakua zimeishia hapa au??

Niambie au nishauri chochote ili niondokane na hii sijui ndio fear of unknown au nini??
Umekopi ama ni wewe? Pole sana
 
Hata mimi ni miongoni mwao isali kwa imani utaona makuu.!!
Ukiweza sali na ya mt Yuda Thadei nayo nzuri.
Ukihitaji muongozo nitafanya kwaajili yako, na nitakuweka kwenye maombi jirani.
Asante jirani,. Niliona mai kuna hadi ya masaa15 ukiachana na hii ya siku 12.. Kama unaifahamu please naomba muongozo🙏
 
Nikiachana na kushika simu means nitakua nalala tu mda wote from morning to night which is tiresome 😌
Simu inakufanya uuchoshe ubongo zaidi, wengi wanaambiwa waache kutumia computer na simu janja kwa muda, hasa wenye matatizo yanayoendana na yako. Mfumo wa masikio hauko sawa, huwezi jua connection yake na uono, pumzisha macho hayo...
 
Simu inakufanya uuchoshe ubongo zaidi, wengi wanaambiwa waache kutumia computer na simu janja kwa muda, hasa wenye matatizo yanayoendana na yako. Mfumo wa masikio hauko sawa, huwezi jua connection yake na uono, pumzisha macho hayo...
Umezungumza kama daktari alivyoniambia,. Yeah ni kweli hata leo from morning sijashika simu ndio nimepatiwa saizi,.. Nitajitahidi Asante
 
Back
Top Bottom