Nishauri chochote niache kuyaogopa maisha

  • Pole sana, ndivyo maisha yalivyo na huo ndio ukubwa; ukisikia nyani mzee amekwepa mishale mingi, inamaanisha kuishi kwake ameweza kupambana na kutegua mitego mbali mbali ya kidunia. unaweza ukawa unateseka alafu wale uliowategemea wakupambanie wanakuwa wanachukulia kawaida sana au wasishughulike na wewe.​
  • Inawezekana pia kukawa na uswahili​
  • Unatakiwa upate mtu wa kukushika mkono na kukufariji, sasa hii itategemea na ndugu wanaokuzunguka, mme/mchumba, majirani n.k​
  • Nb: Katika kupigania uhai, tumia mbinu zote za kivita, iwe hospitali, maombezi, mitishamba n.k​
 
Barikiwa sana mkuu
 
Asante kwa ushauri mzuri rafiki,. Barikiwa sana
 
Nakushauri hivi, ''In whatever you do, always do your best''.

Hata kama ni kufanya mapenzi. Nitakuja baadae kufafanua.kufafanua.
 
Umejaribu kum-consult Mwamposa?.. yupo kawe hapo wewe upo wapi kwani?
 
Una umri gani kwa sasa? Umeolewa au hujaolewa tueleze kodogo mahusiano yako upate ushauri
 
Ukirelax ukajua una muda wa kurekebisha makosa utaishi kwa amani zaidi

Hio biashara kama uliianzisha ww mwnyewe basi omba uzima kwanza

biashara kama ulianzisha mwenyewe na ikaenda vizuri ukipona hutashindwa kuirudisha kwenye mstari😁
 
Pole sana mamy na Mungu wa mbinguni akuponye. Nilikuwa nakushauri hayo mambo ya kuwaza biashara uyaache kwa sasa na kuamini kila kitu kitaenda tena sawa afya yako ikiimarika. Hapa ukichanganya ugonjwa na mawazo ya biashara utasababisha magonjwa mengine kuibuka kitu ambacho si sahihi. Pigania afya yako kwanza na amini Mungu ana kusudi na maisha yako na utakuwa sawa kama mwanzo. Naomba ukazie kwa kusoma isaya 53:5. Utakuwa sawa naamini kwa uwezo wa Mungu kupitia mwanae Yesu Kristo.
Mungu akupe wepesi upone haraka my dia.
 
Kifo,maradhi,huzuni, na HOFU hivi vitu havipo nimatokeo ya ubongo kushindwa kutambua au kupata tafsiri sahihi juu ya kipi sahihi nakipi kisicho sahihi.
Kwenye hayo mabano ndio hutufanya tuone mambo yasio kua kawaida kuyaona kawaida.
Mambo ya miujiza na na uchawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…