Nishawishi kwanini nijenge nyumba na huku sina familia

Nishawishi kwanini nijenge nyumba na huku sina familia

Acha ujinga wewe! Unataka kujenga katika umri wako huo wa miaka 27 ili ugundue nini? Life begins at 40! Kula maisha kijana.

Ukifa kabla ya 40, msiba utafanyikia nyumbani kwa wazazi wako.
 
Ni swala la wakati na muda tu , hizo pesa unazipata kwa wakati siku zinakuja ambazo utahitaji kujenga upatikanaji wa pesa utakuwa mgumu kwako. Hapo ndipo utaanza kukumbuka wakati huu
 
Kwa mfano ingekuwa Ni wewe umri 27 una kazi ya kipato Cha wastani chenye kukuwezesha kuanza ujenzi polepole Ila kwa kujibana bana Kuna ulazima wowote wa na kuanza kufikiria kujenga ikiwa huna mke Wala mtoto na pengine ndugu yako wa pekee tayari Ana maisha yake kaoa huko mbali na bahati mbaya wazazi wako nao wamefariki.

Na ukizingatia huna uhakika Sana Kama utakuja kubahatika kupata mtoto kwa kuwa hupendelei Sana kuoa yaani hujawaza bado kuanza kutafuta mke Ila mambo yako mengine yanaendelea fresh tu.nambie kipi kingine Cha kukushawishi mpaka ujenge Kuna faida gani haswa za kujenga wakati mahali ulipo Tanga wilaya fulani gharama za kupanga Ni nafuu.
Kama uwezo upo jenga, haijalishi utaoa baadae au lah. Baadae utakuwa na kwako, hulipi kodi.
 
Kama unahela ya kujengea na unafikiri gharama za ujenzi hazitakuumiza ni bora ujenge. Jenga nyumba ya kibiashara,Kama si ya biashra Jenga simple house..Nyumba ni asset nzuri kwani mambo yako yakienda kombo kwa baadae inaweza kuwa amana kwenye taasisi za kifedha(mikopo).
Kumbuka majukumu yakianza(familia) utashndwa hata kuserve elfu 10 kwa mwezi.
 
Kama una kipato na huna majukumu, huo ni wakati muhimu zaidi kujenga.

Kuna ile nyumaaaaaaz geukaaa!!!!

Wa mbele anakuwa nyuma, wa nyuma anakuwa mbele!
[emoji41][emoji41][emoji41][emoji1241][emoji1241]
 
Kama una kipato na huna majukumu, huo ni wakati muhimu zaidi kujenga.

Kuna ile nyumaaaaaaz geukaaa!!!!

Wa mbele anakuwa nyuma, wa nyuma anakuwa mbele!
[emoji41][emoji41][emoji41][emoji1241][emoji1241]
Sisi Waislam tunafundishwa kuwa na mambo matatu ni ibada/stara kubwa sana (hautadhalilika)...
1. Miliki Chanzo cha kipato
Chako mwenyewe
(biashara).

2. Miliki Nyumba yako
mwenyewe (Faragha).

3. Miliki Usafiri wako
mwenyewe.
Hata baiskeli tu!
 
Huo umri anytime unaweza kumpa mtu mimba… kupata mwanamke atayetaka umuoe na sometimes yy akakwambia atasimamia shughuli yote ya ndoa.. huo umri anytime unaweza pata hela za kutosha… kma unafikiria kujenga wewe jenga. Wakina robinho walioa wakiwa wadogo wana majumba. Wakina diamond wakina ally hapi.. wakina makonda.. wewe unataka nn cha zaidi dogo. Jenga.
Au hela unaona ujanja zte kuisha kidimbwi na boardroom. Jenga…zalisha…piga vyombo. Oveeer!!
Hujamuelewa....huyo hana uwezo wa kumtia mimba mwanamke...hivyo hana haja ya kujenga
 
Kwa mfano ingekuwa Ni wewe umri 27 una kazi ya kipato Cha wastani chenye kukuwezesha kuanza ujenzi polepole Ila kwa kujibana bana Kuna ulazima wowote wa na kuanza kufikiria kujenga ikiwa huna mke Wala mtoto na pengine ndugu yako wa pekee tayari Ana maisha yake kaoa huko mbali na bahati mbaya wazazi wako nao wamefariki.

Na ukizingatia huna uhakika Sana Kama utakuja kubahatika kupata mtoto kwa kuwa hupendelei Sana kuoa yaani hujawaza bado kuanza kutafuta mke Ila mambo yako mengine yanaendelea fresh tu.nambie kipi kingine Cha kukushawishi mpaka ujenge Kuna faida gani haswa za kujenga wakati mahali ulipo Tanga wilaya fulani gharama za kupanga Ni nafuu.
Nikushauri kwa kutolea mfano wa maisha ya nyoka!
Nyoka katika maisha yake yote hujikoboa ngozi yake na kuota nyingine, kwa muendelezo huo maisha yake yote.

Mfano huo kwa binadamu ni kufikiri na kuwaza.

Unachokiwaza leo kwamba hakina umuhimu kwa sababu zozote zile, kesho waweza kuwaza kitu kilekile na kukiona umuhimu wake.

Jambo la kujenga, ile kulifikiria peke yake na kuanza kulichambua, ni hatua moja kubwa sana ya maendeleo nikupe hongera.

Hakuna binadamu aliyejaliwa kipato asiyetaka kuwa na kwake.

Kwako ndiyo utambulisho wa utu wako na heshima yako.

Kuwa ama kumiliki nyumba hakujalishi idadi ya watu tegemezi kwako, hata ukiwa mwenyewe msimbe, kama umejaliwa kipato, chonde chonde jenga kwanza kabla haujaanza kufikiria jambo jingine.

Fursa ya kipato uliyonayo leo kesho waweza kuikosa.
Kwa gharama za ujenzi zilivyo kubwa nchini kwa sasa hautaweza kuzikidhi kama hautakuwa na kipato cha maana.

Pia kumbuka kuna umri ukifika utakusononesha sana kuishi nyumba ya kupanga inayomilikiwa na vijana wadogo na kisha kuanza kupangiwa masharti ya kipangaji.

Labda uombe Mungu akuue mapema kabla ya kuufikia uzee ukiwa bado mpangaji.

Hela huwa hazifugwi kama ng'ombe, zina mtindo wa nguvu chanya kurudi zilikotoka na kukuacha ukiwa mikono mitupu.

Kuna wakati utafika, pesa hauna ya kuweza kumudu hata kulipia pango na nyumba unayomiliki pia hauna.

Unataka maiti yako ihifadhiwe na kuagiwa nyumba ya kupanga?

Sasa kupanga ni kuchagua na uamuzi ni wako.
 
JENGA haraka sana ukipata UWEZO huo.
Na pia kama umeshafikia umri/kuzid umri wa kuanza familia.

Maana hujui kesho kuna nini.
Unaweza pata ajali. Unaweza kurogwa, unaweza ukafukuzwa kazi, unaweza ukatumbukia kwenye uraibu mwingi ambao ukakudidimiza.

Wakati ulionao ni huu. Na Wakati ni sasa.

Unaweza puuzia mambo sasa kwasababu unajua una muda na hela.

Ila jua Hela huisha, wakati huyeyuka na Majanga utokea.

Kama una muda/hela fanya linalowezekana kimaendeleo, hasa fixed assets.

By the way: nadhan hutak uhuru.
Kujenga ni privacy, maana unaamua ujenge vip na uishi vipi.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ukiangalia upande mwingine.
Kwenye kujenga.

1. Ni nyumba aina gan anaweza kujenga.
Unakuta mtu akiamua kujenga, anaweza kujenga ndan ya wiki moja.
Sio kwasababu ana hela, La hasha.
ila kwasababu (mazingira aliyopo) materials, nguvu kazi na aina ya nyumba anayotaka anaweza kujenga kirahisi.

2. tufanye linalowezekana kwa wakat.
Kama hujisikii kufanya hayo, angalia wanaoendana umri na wewe, je wanafanya/hawafanyi.
Ukitathimi, then wape wale wengi.

Hasa kwenye suala la kimaendeleo kama nyumba.

Ila kama ww ni 20 yrs , na wenzako wote wanaokuzunguka hawana nyumba, ninakuelewa Papaa.
 
Kujenga ni uoga wa maisha bro kula biaaa
Na nyie wenye ushauri hasi utakuta mlishayapatia maisha siku nyingi na mnaishi makwenu na familia zenu raha mustarehe bila wasi wasi.

Lakini kusema mshauri wenzenu vitu vya maana walau wawe kama ama wawasogee, nyie hamtaki mnatibua!

Ninadhani ni kuwa na zile roho za korosho zilizopindia kushoto.
 
Huyu Mnywaji mwenzangu , hana shida na mtu.

Mumuwacheee! [emoji482][emoji482][emoji482][emoji482][emoji482] Dinazarde

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom