Nishawishi kwanini nijenge nyumba na huku sina familia

Nishawishi kwanini nijenge nyumba na huku sina familia

usijenge maana lazima utanunua mabati yakikukata je alisikika kijana wa ovyo kavaa vindala na soksi huku ana iphone na Earphone za wireless masikioni
 
Sio lazima kila mtu ajenge. Ndio maana kuna wanaojenga nyumba za wapangaji.

Kila mtu akijenga nyumba yake nani atapanga?
 
Sio lazima kila mtu ajenge. Ndio maana kuna wanaojenga nyumba za wapangaji.

Kila mtu akijenga nyumba yake nani atapanga?
Atapanga ambae hana uwezo wa kujenga.

Nadhan kila mtu muda na wakat ukifika awe na kwake. Ndio dunia inavyotanuka.

Hata kama ni km kadhaa mbali ya mji.

Ni kwako.

Ukikua ,utajua.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
tz ndio nchi ambayo usipojenga, watu wa jamii yako wanakuzungumzia vibaya.
Kama unauwezo wa kuwa na kwako ma huwi na kwako, watu watazungumza.

Kama una uwezo wa kupanga na haupang, watu watazungumza.

Kama una uwezo wa kuzaa na hauzai,watu watazungumza.

Mama unauwezo wa kuoa/kuolewa na haulewi watu watazungumza.

Ila mara nyingi sio kwa ubaya.
Na vema ukasikiliza,

Lakin kama una sababu ambazo wao hawajui kwann hufany wananyohisi umri/uwezo unaweza kufanya sio makosa yao.

Anyway, ni wawazo yangu

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ukipata ulemavu wa muda wa angalau miaka 2 mfululizo ndipo utajua kwanini mama nitilie wanacheza upatu ili wajenge chumba sebure huko Vikindu.
 
Na nyie wenye ushauri hasi utakuta mlishayapatia maisha siku nyingi na mnaishi makwenu na familia zenu raha mustarehe bila wasi wasi.

Lakini kusema mshauri wenzenu vitu vya maana walau wawe kama ama wawasogee, nyie hamtaki mnatibua!

Ninadhani ni kuwa na zile roho za korosho zilizopindia kushoto.
😅😅😅😅😅😅 bia tamu
 
Nikushawishi wakati mtu mwenyewe ni ndege! Kwani ndege wanakuwaga na nyumba?
 
Labda kama umeamua kutupunguzia stress ila kama nikweli unamaanisha kazi unayo
 
Nakushauri usijenge we kula maisha hayo mengine yatakuja badae,utajengaje kabla ya kuufaidi mshahara bwana!nikushauri mimi ndo nakuja kukaa kwenye hiyo nyumba yako Idiot!
 
Mimi sina familia. Ila Nina nyumba zaidi ya sita nimezipangisha kwa mwezi zinaniingizia zaidi ya m2 .
Mimi mwenyewe ninaishi Kwenye kiappartment cha Chumba sebelu choo na jiko, sinaga wageni nyumbani kwangu.

Nyumba sita + una miaka mingapi!?
 
Nakushauri usijenge we kula maisha hayo mengine yatakuja badae,utajengaje kabla ya kuufaidi mshahara bwana!nikushauri mimi ndo nakuja kukaa kwenye hiyo nyumba yako Idiot!
Mtoto mzuri af nimekupenda Sana umependeza Sana na hio nguo yako ya pink
 
Nyumba sita + una miaka mingapi!?

Mingi ya kutosha plus uelewa mkubwa wa maisha.
Niliwahi Sana kwenda shule degree ya kwanza nimemaliza 2008 nikaajiriwa mwaka huo huo mwanza huko ambapo nilifanya kazi had I 2013 huko nina nyumba maeneo ya buswelu,
2013 nikahamishiwa dodoma ambapo nilikaa miaka 3 huko nimejenga nkuhungu 2017 nikahamia dsm ambapo nimejenga apartment 4 za vyumba 2 vyakulala sebule na choo Kwenye kiwanja kimoja maeneo ya kimara suka.
Dodoma nakiwanja maeneo ya kisasa nilikinunua 2013 just for 1.8 sq Kama 1500 nataka napo nikajenge apartment 8 za kupangisha.
Kilichoniongoza ni uthubutu na kutokuogopa kukopa benki kugharamia ujenzi.
Pamoja na kujibana Sana, Mimi ni yule mtu naweza shinda nyumbani weekend yote Bila kutoka njee na kuna weekends nyingine had I sasahivi naweza nisitumie hata shilingi labda siku ya jumapili Kama nikienda Kanisani nitoe sadaka
 
Hasara za kujenga nyumba
1.utaboreka kukaa sehem moja ila kama umepanga utahama
2.usiombe mafuriko basi jua hilo lako
3gharama za marekebisho ya nyumba kibao
4.watoto na ndugu watakuua ili warithi haswaa ukiwa umetoka familia masikin
Ntarud
 
Back
Top Bottom