Nisipoyasikia haya ndani ya dakika 30 tu za Hotuba yake Mama 'Dodomya' nazima Tv / Redio kwa 'Hasira'

Kwa hiyo kwenye hiyo namba 4 yako, unaamini ni hao akina Mdee pekee wasio na sifa humo Bungeni?

Au ni karibia Wabunge wote tu, hawana sifa za kuitwa Wabunge! kutokana na ukweli kwamba wameteuliwa tu na Hayati kibabe, badala ya kuchaguliwa Wananchi?
MIMI NAONA HAWA CHADEMA WANA UCHU SANA WA KUWA WABUNGE ILHARI WALISHINDWA KWENYE KURA BASI WAJIITE TU NAO WABUNGE WAJENGE NYUMABA WAIITE BUNGE WAWE WANAENDA KUKUTANA HUMO
 
Akiipongeza Simba atanifurahisha na ijumaa ya kesho nitajipongeza na kitu fulani baada ya futari Kwa kuwa aliniudhi aliposema yeye na Magufuli damudamu 😵
Nalog off
 
Hilo la kina Mdee anaruhusiwa kuliingilia kwa sheria ipi hiyo? Mnataka Rais atupe katiba mpya lakini mnamtuma kuvunja katiba aliyoapa kuilinda kwa kuwa jambo linawapendeza.
Kwani hiyo katiba unafikiri kwanini wanaitaka lengo ni kuipunguza nguvu ccm tu hiyo ndio shabaha ya kudai hiyo katiba mpya, usione wanapigia kelele za kuvunjwa katiba ukafikiri wao wenyewe wanaiheshimu katiba hawana kabisa huo utamaduni na ndio kwao hata ikivunjwa ili kufanyika wanayoyapenda wao hawaoni tatizo.
 
Kuja
watu mnavichaaa...
 
8.Kufutwa kwa sheria zote kandamizi.
9.Kurejewa kwa mchakato wa Katiba mpya.
 
Na kuruhusu Bunge kuonyeshwa live.

Pia atoe msimamo wake kuhusu ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo- Maana jiwe alisema tunapigwa
 
Ushuzi mtupu
 
Namba 5 ni fikirishi ina mambo mengi 1.Kulipa madeni ya wafanya biashara wanao idai serikalli 2.Serikali kulipa madeni mbalimbali ya hapa nchini 3.Kuangalia sera ambazo hazina muelekeo (unguided policies) sera nyingi zilikuwa za majukwaani
 
Nini Sasa ulichoandika?
 
Sina maneno mengi sana ila binafsi nilikua ni miongoni mwa wapinzani wa JIWE ambao tulishukuru kuondoka kwake na ni miongongoni mwa wapinzani tuliopata faraja baada ya MAMA kushika kijiti cha JIWE, japo faraja yetu ilikua inaning'inia hewani kwa sababu bado tulikua hatujui muelekeo wa MAMA katika kuliendesha Gari la TAIFA.

Binafsi faraja yangu leo huenda ikakamilika au ikapotea kabisa na kurudi kwenye maisha ya mashaka kama wakati wa awamu ya JIWE. Hii ni kwa sababu kipimo changu leo ni pale MAMA atakapo lihutubia bunge alaasiri ya leo.

Kipimo changu ni rahisi tu ni kwamba MAMA asipo gusia kwa maneno yake mwenyewe katika hotuba rasmi kama ya leo walau kwa kutoa angalizo kwa mlengo wa KUKOSOA au KUTAHADHARISHA au KUKEMEA au KUKOMESHA kama sio KUSITISHA kabisa uwepo wa wabunge wa COVID-19 basi wapinzani wenzangu mjue MAMA atakua sio katika Marais wema ambae yeye ni mmoja wapo tunaemtegemea kurudisha FURAHA na FARAJA ya TAIFA

Hii ni kwa sababu Raisi atakae fumbia macho au kushiriki kuvunja katiba ya nchi basi huyo ni Raisi MDHALIMU kama WADHALIMU wengine tu.

Kwa uzi wangu huu ni ruksa kuzomewa kudharauliwa na kubezwa na wana LUMUMBA karibuni sana
 

Cdm waende vipi mahakamani wakati katiba iko wazi kuwa mtu akifukuzwa chama, automatically sio mbunge? Una uhakika rais hawezi kuingilia bunge?
 
Namba 4 rais ana uwezo wa kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi mpya lakini hana uwezo wa kusimamisha ubunge wa mbunge.

Bunge ni mhimili ulio chini ya Spika.

Rais anaweza kuzoza tu kwamba ubunge huu una mushkeli, lakini hawezi kuwasimamisha ubunge wabunge, hata wale aliowateua mwenyewe.
 
Endelea tu kumuomba israel wako maana leo hata hatasikia maombi yako na rais hatafanya unavyotaka.
 
Hatayagusa yote atayagusa baadhi. Ridhika na machache atayogusa na usimshurutishe "Israeli"
 
All ni all, hata kama atakuwa ni mbaya kiasi gani, ila hatokuja amfikie mtangulizi wake! Aisee yule alipitiliza!!! 😇
 
MIMI NAONA HAWA CHADEMA WANA UCHU SANA WA KUWA WABUNGE ILHARI WALISHINDWA KWENYE KURA BASI WAJIITE TU NAO WABUNGE WAJENGE NYUMABA WAIITE BUNGE WAWE WANAENDA KUKUTANA HUMO

Nimecheka kishenzi ulichoongea hapa ww msichana. Cdm walishindwa uchaguzi au yule shetani aliyeko motoni ndio alinajisi uchaguzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…